Monday 30 June 2014

UNAFAHAMU NI KWA NINI SAFU HIZI HUITWA SAFU ZA MILIMA LIVINGSTONE?

Picha ya safu za milima livingstone ukiwa maeneo ya Lufilyo halmashauri ya Busokelo, wilaya ya Rungwe.

Livingstone alitafuta njia ya usafiri kati ya eneo la Watswana na pwani la magharibi ya Afrika hivyo akaanza safari kubwa iliyompeleka hadi Luanda(Angola). Aliporudi alikuwa Mzungu wa kwanza wa kuona maporomoko ya Victoria Falls mwaka 1855. Mwaka uliofuata alifika Msumbiji alipokuta meli iliyompeleka Uingereza.

Livingstone alipokelewa kama mshujaa kwa sababu taarifa zake zilisababisha kuchorwa upya kwa ramani za Afrika. Alipata sifa nyingi kama mtaalamu wa jiografia na mpelelezi. Kitabu chake "Missionary travels and researches in South Africa" ilisifiwa kote. Serikali ya Uingereza alimpa cheo cha konsuli katika Msumbiji akarudi Afrika. Sasa alijaribu kufuata mwendo wa mto Zambezi kutoka mdomo wake akafika kwenye mto Shire na Ziwa Nyasa (Malawi). Safari zilizofuata 1866 zikampeleka hadi ziwa Tanganyika. 1870 alielekea magharibi kutoka Ujiji akafikia mto Lualaba katika Kongo. Aliporudi Ujiji alikutana na Mwamerika Henry Morton Stanley aliyeongoza msafara wa kumwokoa Livingston lakini hali halisi Stanley alihitaji msaada na Livongstone aliweza kumsaidia kupitia marafiki zake wazalendo.

Safari yake ya mwisho ililenga kugundua chanzo cha mto Nile. Hapo Livingstone aliaga dunia mnamo tar. 30 Aprili 1873 katika kijiji cha Chitambo (Zambia). Watumishi wake chini ya uongozi wa Myao Susi walizika moyo wake palepale wakakausha maiti yake wakaibeba hadi Bagamoyo iliposafirishwa kwa meli Uingereza na kuzikwa London katika kanisa la Westminster Abbey tar. 18 Aprili 1874.

Hadi leo kumbukumbu ya Dr. David Livingstone inaheshimiwa mahali pengi pa Afrika. Mahali pafuatapo paitwa kwa jina lake:
·         Milima ya Livingstone katika Tanzania upande wa mashariki ya Ziwa Nyasa
·         Mji wa Livingstonia katika Malawi
·         Mji wa Livingstone katika Zambia
·         Kisiwa cha Livingstone katikati ya maporomoko ya Victoria Falls
·         Maporomoko ya Livingstone Falls ya mto Kongo
·         Mji wa Blantyre (Malawi) umepewa jina lake kutokana na mji Blantyre katika Uskoti alikozaliwa Livingstone.
Chanzo: Wikipedia.



  KARIBU TANZANIA, KARIBU MBEYA.


Saturday 28 June 2014

KARIBU UPUMZIKE KATIKA FUKWE ZA ZIWA LA TATU KWA UKUBWA AFRIKA.


 Nyumba ya kupumzikia uwapo katika fukwe za ziwa nyasa nyumba hizi huitwa msonge.

Muonekano wa wimbi katika ziwa Nyasa.

 Maji ya ziwa nyasa ni masafi kiasi kwamba unaweza kuona mchanga wake.

Pembezoni kuna safu za milima livingstone iliyosheheni misitu yenye rasilimanyi nyingi sana.

Ziwa Nyasa ni moja kati ya maziwa yenye hadhi kubwa sana duniani, Afrika na Tanzania kwa ujumla, Ziwa hili katika makala mbalimbali za dunia limekuwa likishika nafasi kwanzia ya saba (7) hadi ya kumi (10) kulingana na makala husika kwa mfano the times atlas of the world katika orodha yao wanasema ziwa hili ni la tisa (9) kwa ukubwa duniani, kutoka wikipedia ni ziwa la Tano kwa kuwa na kina kirefu sana duniani. katika tovuti ya 10most today ziwa nyasa limewekwa ni ziwa la tisa (9), katika tovuti ya fact monster ni ziwa la kumi (10)  na pia katika maps of the world ni ziwa la (8) kwa ukubwa duniani.

Katika afrika ziwa nyasa ni ziwa la tatu kwa ukubwa, baada ya ziwa Victoria, na Tanganyika chanzo ni wikipedia.

Pia ziwa Nyasa ni moja kati ya maziwa yenye sifa ya kuwa na aina nyingi za samaki ni (zaidi ya 1500).


Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Thursday 26 June 2014

FAIDA ZA MIANZI KATIKA JAMII ZETU.

muonekano wa miti ya mianzi

 kikapu kilichotengenezwa kwa mianzi.

 kikapu kikiwa na mahindi.

 ndani ya hivi vikapu kuna mahindi na sukari.

Mianzi hupatikana katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa mbeya japo kuwa si kwa wingi kama ilivyo mkoani iringa, mianzi inapokuwa hujikusanya pamoja na kuunda kitu kama kamsitu fulani.

Vikapu vyote hapo juu vimetengenezwa kwa mti wa muanzi ambao hukunjwa kwa ustadi kisha kuunda kikapu, vikapu ama vitu vitengenezwavyo kwa mianzi ni imara sana.

Kikapu cha kwanza ni kikubwa hivyo hutumiwa kwa shughuri kadhaa ikiwemo kuchumia chai, pia kama kuku ameatamia mayai yake baadhi ya watu humfunikia kwa kikapu ili asitoke toke nje.

vikapu viwili vya chini hutumiwa katika sherehe ama misiba kwa kubebea vitu mfano hivyo vikapu vitatu vya mwisho ilikuwa ni msibani.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Wednesday 25 June 2014

KIJUNGU JIKO.

kijungu jiko hupatikana katika mto kiwira maeneo ya KYIMO KIJIJI KITULIVU maarufu kama KK, eneo hili lipo wilaya ya Rungwe mkoani mbeya.

Haya ni maneno ya ukaribisho unayokutana nayo kabla hujaenda katika kijungu,

 Ukiwa juu kabla hujashuka katika usawa wa mto, utakiona kijungu kwa muonekano huu baada ya kusogea ndipo utaona vizuri sana.



mara baada ya kushuka hivi ndivyo mto kiwira huonekana kwa uzuri sana.

Hiki ndicho kijungu jiko na hapa ndivyo maji yanavyo ingia, ukiyatizama sana utaona kama yanachemka yakigonga chini.

Baada ya kuingia katika kijungu maji haya hutokeza upande huu kisha kuendelea na safari zake.


kwa mujibu wa mwenyeji wetu alisema mto huu hutiririsha maji yake kutoka mlima Rungwe mpaka ziwa Nyasa, maji ya mto huu yanapoingia katika kijungu yanaingia kwa kasi sana kisha kutokea upande wa pili yake, yakitoka huendelea na safari zake ambapo ni umbali mdogo kutoka eneo la kijungu mpaka lilipo daraja la mungu.

Kijungu jiko ni eneo lenye kustaajabisha sana kwa sababu kimeumbwa kwa mwamba na kufanya umbo la kama la chungu, ambacho hupokea maji yote ya mto huo na kuyapeleka chini bila kuyapitisha juu ya mwamba huo.

Inaelezwa kwamba ili mtu uvuke kwa usalama kwenye mwamba juu ya kijungu kutoka upande wa mashariki lazima atumie mguu mmoja wa kulia kisha kuusogega taratibu mpaka ukimaliza kuvuka, na ukitoka magharibi utatakiwa kutumia mguu wa kushotona kuusogeza taratibu huku mguu wa kulia ukifuata nyuma. kwa kufuata hayo hutatumbukia.

Kitu kingine ni uwepo wa imani kuwa endapo mtu akizama katika mto huo, lazima afuatwe mzamiajai aliyerithi kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo basi aliyezama atakaa katika shimo(mbako) kwa muda wa siku saba na muda huo ndugu mkiwa mtoni usiku na mchana ndipo atakuja kuonekana.

mwenyeji wetu hakuishia hapo alisema kwa mfano ukiwa na shilingi mia ukiirusha katika maji hayo, itakapo gonga maji itarudi na kuanguka pembezoni mwa mto huo na yale maji yaliyotwanyika yatajirudi na kupika katika mwamba ule na si nje ya mwamba.

Namna ya kufika, ukitokea mbeya au kyela unashuka KK kisha utaona kibao cha shule ya gods bridge na kimeonesha uelekeo, utafuata ule uelekea na utatangulia kuona njia panda yenye kuelekea daraja la mungu, ukinyoosha moja kwa moja utavuka eneo la  magereza na kufika kijungu jiko. ukiwa na gari binafsi pia inaweza kufika mpaka pale kipo kile kibao chenye maelezo ya malipo juu ya eneo husika. lakini ukienda daraja la mungu hakuna malipo yoyote.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.






HALI YA HEWA YA MANOW KWA SIKU MBILI ZILIZOPITA.

Baadhi ya maeneo yakiwa yamefunikwa na ukungu mzito.  

 Maeneo ya barabarani pia hali ikawa ni ile ile.

 Majengo ya shule pamoja na majengo ya walimu yakiwa hayaonekani vizuri

ulikuwa huwezi kuiona lwangwa kama ilivyozoeleka siku zote.

Mwezi wa sita ni mwezi wenye baridi sana katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa mbeya, ukiwa katika wilaya ya Rungwe hutakaa ukaacha kuvaa sweta kwa sababu ya baridi yake. 

Haya ni maeneo ya shule ya seminari  manow ambayo kwa muda wa siku mbili wakazi wake hawakubahatika kuliona jua kwa sababu ukungu ulitanda anga.

kwa wale mpendao kubadirisha hali ya hewa mkiyachoka maeneo ya joto, karibuni sana  mbeya japo kwa siku moja upunguze matumizi ya viyoyozi.



MLIMA WA TATU KWA UREFU TANZANIA (MLIMA RUNGWE).

 mlima Rungwe kwa mbali uonekanavyo.

mlima unavyoonekana ukiwa katika mji wa Tukuyu.

ukiwa vijiji jirani karibu na mlima.

Muonekano wa mlima rungwe ambao kwa urefu ni watatu Tanzania ukianza na mlima kilmanjaro  wenye  mita 5,895 ukifuata mlima meru 4,566 na unafuata mlima rungwe  2,960 ambao una, mabwawa yasiyopungua maji wala kuongezeka,  maporomoko ya maji, wanyama mbalimbali wakiwepo na vyula wanaopatikana rungwe tu na nyani aina ya kipunji anayepatikana katika mlima rungwe tu duniani kote. 

Mlima Rungwe ni volkeno iliyozimika ya Tanzania kusini magharibi ikikadiliwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2,000 hadi 5,000 iliyopita. mlima huu una kimo cha mita 2,960 ni mlima mkubwa mkoani mbeya. 

Mlima unasimama juu ya ncha kaskazini ya ziwa nyasa, upande wa kusini mashariki wa mlioma hupokea usimbishaji wa milimita 3,000 kwa mwaka ambao ni juu kabisa katika Tanzania.

Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutuba na kilimo, pia Rungwe ni eneo la wanyakyusa jina la mlima limekuwa pia jina la Wilaya ya Rungwe 



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.



KIPUNJI ( Rungwecebus kipunji )

kipunji akiwa katika mti.

Misitu ya Tanzania ni nyumbani kwa mamia ya spishi za wanyama na idadi kubwa ya wanyama ni wale ambao hujapata kuwaona  mahali pengine dunia kutokana na bahati hii tulio nayo ya kupata viumbe ambao ni nadra sana kuwapata pahala pengine ni wajibu wetu kulinda na kutunza  makazi yao ili kuwasaidia wanyama hawa kuishi miaka mingi.

Uwapo katika mazingira yenye jamii ya nyani hakika utafurahi sana kutokana na namna ambavyo ni marafiki wakubwa wa binadamu, wana michezo yenye kufurahisha sana hususani wakitambua mnawashangaa wana ustadi wao wa kuruka kutoka tawi moja la mti kwenda tawi jingine, michezo mingine ni pamoja na ule wa kuwarushia ndizi kuna namna wanaidaka kwa madoido hakika utapenda mwenyewe.

kipunji ( rungweceubus kipunji) ni jamii mpya ya nyani waliogunduliwa mnamo mwaka 2003, ni aina ya tumbili wanaopatikana na kuishi katika misitu ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania. wanasayansi waliwaita jamii hii mpya Rungweceubus kutokana kwamba wanapatikana katika mlima Rungwe na maeneo mengine yanayoizunguka milima hiyo tu.



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.


Tuesday 24 June 2014

TUKUMBUKE ENZI

   Afrika ina makabila mengi ambayo hayawezi kuhesabika na vikundi vya kikabila na vya kijamii. Baadhi ya vikundi hivi vinaashiria wakazi wengi ambao ni mamilioni ya watu. Vikundi vingine ni vikundi vidogo vya watu elfu kadhaa.

   Tanzania ina mila tajiri ya sanaa, sanaa za Tanzania hujieleza katika aina mbalimbali ya mchongo wa mbao, shaba na matendo ya sanaa ya ngozi. sanaa ya hii pia inajumuisha uchongaji, uchoraji, ufinyanzi, mavazi ya mwili na ya kichwa katika sherehe na mikutano ya kidini n.k 

   kiasili mbeya ilikuwa eneo la wasafwa, siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa wasafwa pamoja na makabila ya wanyakyusa kutoka wilaya ya Rungwe na kyela, wanyiha kutoka mbozi, wandali kutoka ileje na wakinga kutoka makete. lakini kutokana na utandawazi na kuhama kwa watu kutokana na sababu mbalimbali hakika kwa sasa kila mkoa lazima ulikute kila kabila,

   hadithi za mafuriko zilikuwa zikienea katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Kwa mfano kwa upande wa mbeya hadithi ya utokeaji wa ziwa kiungululu, kisiba, ikapu n.k inasemekana  kwamba alitokea mtu mchafu aliyeomba maji katika nyumba kadhaa za jamii hizo na kunyimwa,  lakini alikuwepo mama mmoja msamalia mwema alimtunza na kumpa chakula pamoja na maji. Mungu wake alimtuza kwa kumpa utajiri, alimshauri aondoke kutoka eneo hilo, na kuharibu jirani wake wachoyo. Baadhi ya mila na desturi zilizokuwa zimetawala katika jamii zetu ni pamoja na :-

Kumeza peke ya mchungwa.
Kulikuwa na imani kuwa ikatokea umemeza peke ya mchungwa basi mti utaota katika kichwa chako na wenzio watakuwa wanapanda mtini kuchuma machungwa, lilikuwa ni fundisho kubwa sana ambalo lilitufanya wengi tuwe makini pindi tulapo machungwa ama tunda loloto lenye peke. na ilikuwa kwa bahati mbaya ukameza basi nyumba nziwa watakuimbia nyimbo, watakusema na utakosa raha kipindi chote watakacho kusema.

Kukaa juu ya kinu kisha kuchafua hewa(kujamba).
Ilisemekana ukikaa juu ya kinu kisha ukachafua hewa basi utatokwa na majibu katika makalio yako, kinu kilitumika katika shughuri mbali mbali za jikoni hivyo haikuwa busara kukichafua, ndio maana wazazi wetu walitumia njia hiyo kutufanya tukiogope kinu.

Kuitika Usiku uitwapo na mtu usie mjua.
Ulikuwa huruhusiwi kuitika usiku pindi uitwapo na mtu usie mjua kwani ilisemekana unaitwa na jini hivyo utakapoitika basi utapotea na hutaonekana tena, Na masimulizi ya majini yalikuwa yakitisha sana katika jamii zetu kuwa majini huka watu hivyo ilikuwa ngumu sana kukaidi agizo hili.

Kuongea ukiwa chooni.
Wazee wetu walisema Ukiongea kama uko chooni basi utavimba mashavu, na hautokuja kupona kamwe, lakini maana yake ilikuwa tuwe wasafi maana chooni kuna mambo mengi sana. 

je wewe pia ulipata kuyasikia haya? unaruhusiwa kucomment nasi tutafurahi sana kuona comment yako




Monday 23 June 2014

KITANDA CHA MIANZI

Miti ya mianzi inapatikana kila kona ya bara letu la Afrika, pia Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengi yanayopanda miti ya mianzi. Miti hii ina sifa nyingi sana ikiwemo ile ya kuwa na ugumu wa hali ya juu sana, pia hudumu kwa muda mrefu mara baada ya kukatwa. Jamii nyingi hutumia mti huu katika shughuri mbali mbali mfano kutengenezea nyumba, dari, ua au uzio wa nyumba, kichanja cha kuanika vyombo, vikapu hususani vya kuchumia chai, nk 

kitanda hiki kimetengenezwa kwa mti wa muanzi, pembeni kina stuli zake mbili moja kushoto na nyingine kulia upande wa kichwa ambazo huweza kutumika kama meza.


hapa ni kajumba kadogo ambako huweza kutumika kama sehemu ya kupumzikia, bwana meshack mwakalebela akiwa amepumzika katika kajumba hako. 

vitu vyote hivi (kitanda pamoja na kajumba haka) vimetengenezwa na magereza mbeya, hakika ni ufundi wa hali ya juu sana na vinavutia kwa kuvitazama. 


Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya.


VIDEO YA BAADHI YA VIVUTIO VYA KITALII MKOANI MBEYA.

Kwa wale wapenzi wa picha za mnato (video), kipande hiki cha video kinaonyesha baadhi ya vivutio vya kitalii vipatikanavyo mkoani mbeya, picha ya kwanza inaonyesha namna maji yanavyo ingia na kutoka katika kijungu jiko (cooking pot) kilichopo katika mto kiwira.


Picha inayofuata ni ziwa  Nyasa lililopo wilaya ya kyela maarufu kama Matema Beach, pembeni yake ni mitumbwi ambayo hutumiwa katika shughuri mbali mbali ikiwemo uvuvi. kisha picha ya mwisho inajumuisha ziwa Ngozi lililopo wilaya ya Rungwe katika milima ya uporoto, daraja la mungu lililopo katika mto kiwira, Kimondo kinacho patikana wilaya ya mbozi, na Matema beach  kyela.

unaruhusiwa kupakua video hii kisha kushare na uwapendao.

Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya.
Sunday 22 June 2014

ZIWA KIUNGULULU (CRATER LAKE)

Ziwa kiungululu linapatikana katika halmashauri ya busokelo wilaya ya  Rungwe, liko umbali wa kilomita zisizozidi 48 kutoka tukuyu mjini. ziwa hili lipo eneo liitwalo lugombo katika kijiji cha kabembe kata ya itete umbali mdogo kutoka hospitali teule ya Itete.


muonekeno wa ziwa kiungululu, lililopo lugombo na kwa nyuma ni safu za milima livingstone iliyopo lufilyo.

Hakuna mto wowote unaoingiza wala kutoa maji katika ziwa kiungululu, ziwa hili lina samaki kiasi wakubwa kwa wadogo, ukitizama kwa mbali utaona safu za milima livingstone iliyoambaa mpaka katika kingo za ziwa nyasa.

Katika masimulizi ya kihistoria juu ya utokeaji wa ziwa kiungululu inasemekana, kulikuwa na mtu mmoja alitoka sehemu za mbali sana na kufika mahali hapa, alipofika alionekana kuwa ovyo sana kwa maana ya kwamba alikuwa mchafu sana, aliingia katika nyumba ya kwanza kuomba maji ya kunywa kutokana na hali aliyokuwa nayo ya uchafu walimkatalia, basi akasogea katika nyumba ya pili vivyo hivyo wakamkatalia na kumfukuza. lakini alipofika katika nyumba ya tatu alimkuta mama mmoja msamalia mwema ambae alimuonea huruma na kumpa maji ya kuoga, akamvisha nguo zingine na kisha kumwandalia chakula, mara baada ya kumaliza kula ndipo yule mtu akamwambia mama yule uhame mahala hapa uhamie sehemu nyingine kwa maana hapa patatokea maajabu, wale watu walipomwona mama yule anahama wakamsema na kumtukana kwa kusema kichaa anamhamisha na kumuona kama mtu asiekuwa na akili, baada ya kutii agizo lile ikawa kama pigo kwa wale watu waliokuwa wamebaki. Pakadidimia na kisha yakaibuka maji.

Masimulizi hayo yalitumika ili kutoa elimu kizazi hata kizazi kuzifanya jamii kuwa na ukarimu, maana masimulizi hayo hayo yalitumika hata katika maeneo mengine mfano kisiba, ikapu, ilamba na kingili.

lakini kijiografia inasemekana ziwa kiungululu lilitokana na mlipuko wa kivolkano mfano wa mzuri ni ziwa ngozi, kisiba n.k.

karibu sana Tanzania, karibu Mbeya.

HISTORIA FUPI YA MKOA WA MBEYA

   
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, Iringa na Ruvuma. Mkoa wa Mbeya ulianzishwa mwaka 1961 na ulikuwa ukijulikana kwa jina la ‘Southern Highland Province’ kwa kujumuisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa na Rukwa. Mkoa una eneo la km. za mraba 63,617 Kati ya hizo km. za mraba
61,783 ni za nchi kavu na km. za mraba 1,834 ni eneo la maji.

Kulingana na Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 1967   mkoa ulikuwa na watu 969,053, Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 Mkoa wa Mbeya ulikuwa na jumla ya watu 2,063,328. Kufikia mwaka 2010 mkoa ulikadiriwa kuwa na watu 2,662,156. 

Mkoa wa Mbeya upo kusini magharibi mwa eneo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mkoa upo katika Latitudi kati ya 7º na 9º 31’ kusini ya Ikweta na Longitudo kati ya 32º na 35º mashariki ya Greenwich. Mkoa unapakana na nchi za Zambia na Malawi upande wa kusini, Mkoa wa Rukwa upande wa magharibi, Mikoa ya Tabora na Singida kwa upande wa kaskazini ambapo kwa upande wa mashariki unapakana na Mkoa wa Iringa. Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Mbozi na Kasumulu katika Wilaya ya Kyela, hufanya milango ya kuingilia na kutokea nchi za Zambia na Malawi.

Katika enzi za ukoloni wa Waingereza, Mkoa wa Mbeya ulikuwa ukijulikana kwa jina la ‘Southern Highland Province’. Mkoa ulikuwa ukiunganisha baadhi ya maeneo ya mikoa mitatu ya sasa ambayo ni Iringa na Rukwa. Jina la Mbeya limetokana na neno la kisafwa "Ibheya" ambalo maana yake ni chumvi, kutokana  na  wafanyabiashara  kufika  na  kubadilishana  mazao  yao  kwa chumvi. Mji wa kisasa wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa. Mkoa huu ni moja kati ya mikoa mikongwe tisa (9) iliyokuwepo mpaka wakati wa uhuru mwaka 1961.


Katika kipindi hicho, makabila makuu katika Mkoa wa Mbeya yalikuwa ni Wasafwa, Wanyakyusa, Wandali, Wasangu, Wamalila, Wanyiha, wakimbu na Wanyamwanga.


Kijiografia, Mkoa ulianzishwa katika maeneo yanayojulikana hivi sasa kama Uhindini, Uzunguni na Majengo. Mji ulipangwa kufuatana na kawaida ya miji ya kikoloni ya Afrika Mashariki kuwa na sehemu tatu zifuatazo;

(i)       Uzunguni kama sehemu ya nyumba za Wazungu na kando yake ofisi za serikali (Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Polisi na Mahakama)

(ii)      Uhindini   kama   mtaa   wa   biashara   uliokuwa   mikononi   mwa wafanyabiashara wenye asili ya Kihindi na Kiingereza;

(iii)     Majengo kama sehemu kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika na familia zao.

Kwa upande wa masuala ya kiimani, Mkoa ulikuwa umegawanywa kama ifuatavyo;

(i)       Kanisa Anglikana lililokuwa dhehebu rasmi la Uingereza ambalo lipo chini ya eneo la Uzunguni karibu na ofisi za kiserikali kama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mahakama.

(ii)      Kanisa  la  Moravian  la  mjini  lilijengwa  eneo  la  Majengo  iliyokuwa sehemu kwa ajili ya makazi ya Waafrika.

(iii)     Kanisa Kuu Katoliki lililokuwa maeneo kati ya Uzunguni na Uhindini karibu na Majengo ambalo lilihudumia Wazungu wachache hasa Waeire na Wahindi kutoka Goa na Waafrika wachache.

Kwa upande wa masuala ya uchumi Mkoa wa Mbeya ulitegemea kilimo cha mazao ya chakula yakiwemo mahindi, viazi vitamu, mtama, mpunga na ndizi. Shughuli nyingine zilikuwa ni biashara na viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza zana za kilimo.


Kielimu, shule zilizokuwepo zililenga hasa kutoa elimu kwa watoto wa machifu, wazungu na wahindi. Shule hizi zilikuwa zinamilikiwa na serikali na mashirika ya dini.  Shule za serikali zilijulikana kama ‘Native Authority’ na za mashirika ya dini ziliitwa shule za wamisionari. Waalimu wazalendo walikuwa wachache, wengi wao walikuwa ni wazungu. Misheni ya Rungwe ndiyo pekee iliyokuwa na Chuo cha Elimu katika Mkoa wa Mbeya baada ya uhuru.


Kuhusu huduma za afya, jamii kwa kiasi kikubwa ilikuwa inatumia tiba za kienyeji. Hospitali zilikuwa chache zikitoa huduma bure isipokuwa hospitali za wamisionari.

Historia hii inapatikana katika taarifa ya mkoa wa mbeya miaka (50) ya uhuru.

karibu sana Tanzania, karibu Mbeya

KIMONDO CHA MBOZI.

Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 12, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya, Tanzania.
Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.
Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8,69%, sulfuri0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Kina muonekano mithiri ya jiwe lakini ajabu yake ni pale utakapo kigonga kinatoa mlio kama wa debe tupu.
Muonekano wa kimondo hicho kilichopo mkoani mbeya, katika wilaya ya mbozi. 

jiwe hili la chuma kwa ukaribu huonekana hivi.

hapo ni kama kachungu kana maji ukiyagusa ni ya baridi sana kama yametoka katika jokofu

Eneo hili wataalam wa mambo ya jiolojia walikata kipande cha jiwe la chuma hicho ili kufanyiwa utafiti. 

    Kimondo hiki kipo umbali wa kiasi cha kilometa 70 kutoka Mbeya mjini, kusini mwa Tanzania, katika barabara kuu ya Tanzania-Zambia, njia kuu ya kwenda Tunduma.
Hakuna anayejua kimondo hicho kilianguka lini, lakini lazima iwe kilianguka zamani sana kwani hakuna hekaya zozote kukihusu. W. H. Nott, soroveya kutoka Johannesburg, aliandika kwamba aliona kimondo hicho mnamo Oktoba 1930. Tangu wakati huo, mtaro ulichimbwa kukizunguka, na kufanya kionekane kana kwamba kimeinuliwa na kuwekwa juu ya madhabahu ya mawe. Hivyo, kimondo hicho kimebaki mahali kilipoanguka.
Watu fulani wamejaribu kukata sehemu fulani ya kimondo hicho ili kujiwekea kama kumbukumbu, lakini hiyo ni kazi ngumu sana. Mnamo Desemba 1930, Dakt. D. R. Grantham wa Chama cha Jiolojia alipojaribu kukata kisehemu cha karibu sentimeta kumi kwa msumeno, ilimchukua muda wa saa kumi! Kisehemu hicho kinaweza kuonekana katika mkusanyo wa vimondo kwenye Jumba la Makumbusho la Uingereza huko London.

Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya







Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts