Tuesday 17 June 2014

ZIWA MASOKO/ KISIBA




Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani dakika 40 au 50 kwa gari.
Kihistoria inasemekana wajerumani walipokuwa wakifukuzwa na waingereza walitupa pesa na baadhi ya vitu vya thamani katika vita ya kwanza ya dunia. 

Bwana benson mwaipopo ambae amekulia hapa alikuwa na mengi ya kutueleza ambayo ni:-

  • ziwa masoko linapatikana kata ya kisiba na tarafa ya pakati, hapo kisiba palikuwa na vituo au sehemu za kuogea kama ifutavyo kulikuwa na sehemu ya masoko, resthouse, lwifwa, mibula na sehemu zingine lakini hizo sehemu zilikuwa maarumu kwa sababu zilifanyiwa uchunguzi zikaonekana zina kina kifupi cha maji lakini sehemu iliyokuwa na kina kifupi zaidi ni sehemu ya lwifwa ambako pia kabla hujafika majini kuna sehemu ina uwanja hapo ndipo wazungu walikuwa wakija kutarii na kufanya uchunguzi wake huwa wanafikia eneo hilo la lwifwa na eneo la bomani ndiko yanapatikana makaburi matatu na makaburi hayo yapo kwa ajili ya ukumbusho kwamba kuna wajerumani walikufa maeneo hayo walipokuwa wanaondolewa na wakoloni na inasadikika kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya nyoka mmoja mkubwa na mjerumani huyo nyoka alikuwa na vichwa viwili walipambana sana.
  •  Inasemekana kwamba katikati ya kina cha maji pana joka kubwa sana lipo chini ya maji na chungu kimoja pamoja na sanduku lililo jaa Rupia kama tujuavyo rupia ni kitu kimoja cha ajabu sana inasomekana inatumika kwa waganga wa kienyeji na huwa kama majini hivyo basi mnamo mwaka 1996 mwezi wa 8 wazungu walikuja kufanya utafiti wao waliweka mashine zao katikati ya maji ili kuweza kufanikisha kuchukua sanduku lililopo hapo, matokeo yake wakamtuma mzungu mmoja kati yao azame chini akaangalie atafunga vipi lile box la rupia akashimdwa alikuwa anaitwa Mark akaleta picha alizopiga pale chini na udongo alioleta kiujumla pana maajabu sana. 
  • Ifikapo saa 12 jioni katikati ya bwawa huwa panatokea mstari mmoja, unaotoka lwifwa kuelekea bomani usawa yaliko makaburi yale matatu. Huwa unakimbia kwa kasi ya ajabu ukizubaa huwezi ukauona unakuta tayari umejigawa unabaki kushangaa upande kunakuwa na mawimbi na upande kunakuwa na maji yaliyotulia bila hata chembe ya wimbi upande huo ambao hauna mawimbi kunakuwa na samaki sana japo ni vile vidogo vidogo ila vitamu sana basi upande wa pili huwa hawapatikani kwa wingi kuna wazungu walikuja mwaka 1997 wakapandikiza samaki wakubwa baada ya kugundua kuwa lile bwawa lilikuwa linaupungufu wa samaki lakini samaki hao walikuwa wakali sana wakiwaona wenyeji wanawatimua au ukiweka miguu majini unakuta wanakutafuna yani hapo bwawani panafurahisha hadi raha. 

    Like page yetu facebook, pia tu follow instagram kwa mbeya home of tourism
    pia tuandikie maoni katika sanduku letu pembeni

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts