Sunday 6 July 2014

HISTORIA FUPI YA WASAFWA.


Jamii kubwa kuliko jamii zote katika wilaya ya Mbeya ni Wasafwa. Wasafwa huishi katika milima ya Mporoto Kaskazini ya mlima Rungwe na katika bonde ambalo laenea kati ya milima ya Mbeya upande wa Kaskazini na milima ya Umalila na Unyiha kwa upande wa Kusini na Kusini Magharibi. Mali kadhalika, Wasafwa huishi upande wa Kaskazini wa mlima Mbeya na katika sehemu ya uwanda wajuu unaopakana na Wilaya ya Chunya.

Wasafwa wanazungukwa na jamii hizi:- Wasangu upande wa Kaskazini, Wanyiha upande wa
Magharibi, Wamalila upande wa Kusini-Magharibi, na Wanyakyusa kwa upande wa Kusini.

Wasafwa hawajapata kuwa chini ya Utawala wa namna moja, bali walikuwa wametawaliwa na machifu mbali mbali. Machifu wa Kisafwa waliokuwa wanajulikana sana tokea karne ya 19 ni


Mwalyego ambaye alijenga nyumba yake kwenye miteremko ya milima ya Mbeya karibu na Utengule, Chifu Lyoto alitawala  sehemya mteremko  wa mlima Mbeya upande wa Usafwa  ya Kaskazini kuelekea  bondla Usangu,  Zambalitawala  sehemu  ya upande  wa Kaskazini  - Mashariki  za miteremko ya milima ya Umalila, Malema alitawala sehemu za Kaskazini - Mashariki za miteremko ya milima ya Unyiha.


Ingawa ni vigumu sana kujua chimbuko la Wasafwa lakini koo mbali mbali za Wasafwa zakumbuka wapi zilitoka. Chimbuko la Wasafwa limo katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni ile inayowahusWasafwa ambao asili yao ni Ugogo. Ziko sababu nyingi ambazo zilisababishkwa Wagogo fulani kwenda kuishi sehemu za Usafwa na kuoana na Wasafwa. Nchi ya Mbeya ilikuwa na rutuba nyingi kwa kupanda mazao ya chakula, biashara ya utumwa ambayo iliendeshwzaidi na Waarabu, na kadhalika. Msafara wa watumwa ulifuata bonde la Usangu kuelekea sehemu za pwani ambako ndiko yalikuwako masoko ya kuwauzia hao watumwa. Njia hii ya watumwa ilifuatwa wakati njia ya kupitia Ugogoni ilipoonekana ni ya gharama kubwa sana kwa wafanya biashara hii na wakati mwingine  ilifungwa  na jamii za Kigogo  kwa sababu  mbali mbalza kutoelewana  na Waarabu, Wafanya  biashara.  Na kamtunavyoelewa  machifu  wa Kiafrika  nao walijitupa  barabara  katika biashara hii na kuwauza wenzao. Kwa hiyo, Wagogo waliokwenda  sehemu za Mbeya yawezekana walifuata biashara halafu baadaye wakafanymastaakimu  yao pande hizi za Mbeya na kuweza kuoana na Wasafwa wa huko na baadaye watoto wao wakafuata malezi ya Kisafwa na kuwa Wasafwa Kamili. Pengine hao Wagogo walikwenda sehemu hizo za Usafwa kwa sababu ya kukimbia taabu ya kutiwa utumwani na Waarabu kwa sababu njia kuu ya biashara ya utumwa ilipitia katika nchi yao.


Chimbuko jingine la Wasafwa ni Ukinga. Hasa hili ndilo chimbuko kubwa la Wasafwa ambao kwa mila na desturi wanafanannao sana. Wasafwa wanatoa sababu kubwa iliyowafanya  waje sehemu hizi za Mbeya nayo ni sababu ya kupata moto. Kama inavyosimuliwa na wazee wengi wa Kisafwa, watu wa asili waliokuwa wanakaa pande za Mbeya, walijua jinsi ya kutengeneza moto, na Wasafwa wengi wakafuata utaalam huo toka pande za Ukinga na baadaye wakafanya maskani yao huko pengine baada ya kuwafanyia vita wenyeji wa huko halafu wao Wasafwa ndio wakawa watawala wa nchi yote ya Mbeya. Kwa kawaida Wasafwa wana desturi ya kukoka moto mmoja halafu huo moto huenea nchi nzima ya Usafwa. Moto huu ulikokwa kwa kufuata sherehe maalum.

Chimbuko la tatu la Wasafwa ni Unyakyusa na pande za Kaskazini za Malawi - Karonga. Kwa mfano, chifu Mwalyego ambaye baadaye alifanywa na Wajerumani kuwa chifu mkuu wa Wasafwa katika mwaka wa 1898 yeye husimulia kuwa asili yao ni Karonga na baba mkubwa wa Mwalyego (great grand father) Bwana Shyungu aliishi Karonga na utawala wake ulienea sehemu yote ya nchi ya Ukonde. Mtoto wake Mwamwondo alifanya maskani yake Nshorongo sehemu iliyo karibu na milima ya Igale. Mtu huyu alioa wanawake wengi na pia alioa binti ya Chifu Lyoto ambaye alitawala Usafwa wakati huo. Baadaye Mwamwondo akaasi na kumpindua mkwewe na yeye akawa ndiyo mtawala wa sehemu  hii ya Usafwa.  Mwamwondo  alizawavulana  wengiMwamparandje,  Mwenipyana  na Nsewe. Mtoto huyu Nsewe alizaliwa na mke wa Mwamwondo ambaye alikuwa binti ya Lyoto. Mwamwondo alifariki dunia mara baada ya Nsewe kuzaliwa. Mwamparandje akatawala nchi ya Nshorongo badala ya baba yake. Walakini ndugu yake Mwenipyana alipigana na Mwamparandje na akamshinda. Kwa hiyo Mwenipyana akatawala sehemu ya Nshorongo na Mwamparandje akakimbilia katika milima ya Igale.


Wasafwa walimkataa Mwenipyana kwa sababu mama yake hakuwa Msafwa na pia tabia yake mbaya ilimfanya asikubaliwe kutawaia. Wakati Wangoni walipoingia Mwenipyana aliwasaidia Wangoni kwa kuwapa chakula ambacho raia wake walikihifadhi. Tabia hii iliwaudhi sana Wasafwa, kwa hiyo wakamkataa kuwatawala.


Mwamwondalipofariki mke wake, binti Lyoto alirudi kwa baba yake pamoja na mtoto wake Nsewe. Nsewe alipokua, babu yake Lyoto alimteua Nsewe kuwa chifu badala ya baba yake - Mwamwondo.  Baadaye  Nsewe  akamwasi  babyakna akapigana  naykalazimika  kukimbilia milimani alikofia wakati wa majilio ya Wangoni. Nsewe alizaa watoto wengi:- Mwalyambi, Zambi, Milambo, Ngaja, Nswila, Mpoli, Mwansonswe, Mwembe, Sidjodjo, Djedjo na Mudjenda. Nsewe aligawanya sehemu ya Utawala wake na kuwagawia watoto wake hawa.

Wasangu chini ya chifu Merere walipoingia katika nchi ya Nsewe, Nsewe alikufa wakati wa vita  na watoto  wake  wakatoroka.  Nswila  allkwenda  Ukonde,  Zambakakimbilia  Unyamwanga  na watoto wengine wakajificha chini ya machifu wengine. Nswila hakukata tamaa na kwa msaada wa machifu wa Unyamwanga na Unyiha, akawashambulia Wasangu na akawashinda na kuwatoa toka nchini mwake. Nswila alipotuliza nchi yake, ndugu zake wote wakarudi toka walikokimbilina wakamheshimu  sana kwa kitendo alichokifanya  cha kuwafukuza  Wasangtoka Usafwani,  lakini hawakumkubali kama yeye ndiye chifu mkuu wa Usafwani. Badala yake kila mmoja wao alitawala sehemu aliyopewa na baba yao Nsewe.

Chanzo: safarilands.org katika makala ya jamii ya wasafwa. 


Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts