Saturday 5 July 2014

HISTORIA YA WANYAKYUSA.



Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI?
Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza. Fasili hii ni nzuri na inajitosheleza kwa maana kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa.

Hivyo basi asili ya wanyakyusa bado ni mjadala mrefu ambapo wataalamu/wazee mbalimbali wanahitilafiana juu ya asili au chimbuko lao Kama ilivyo katika kiswahili kuwa na nadharia kadhaa juu ya asili na chimbuko la kiswahili pia vivyo hivyo kwa wanyakyusa, inawezekana ulisikia kitu kama hiki au kingine usisite kucomment katika ukurasa wetu wa maoni juu ya ujuacho.


(Kwa mujibu wa wikipedia) Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni kabila la watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) kaskazini kwa Ziwa Nyasa.
Lugha yao, inayoendelea kutumika sana, ni Kinyakyusa.
Mara nyingi Wagonde upande wa kusini wa mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Mwaka 1993 watu zaidi ya milioni walikuwa wanajumlishwa kwa jina hili, takriban 750,000 upande wa Tanzania na 300,000 upande wa Malawi.


Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde, ambao kati yao Wanyakyusa walikuwa ndio kabila kubwa. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" limekuwa jina la kundi kwa jumla.
Hadi leo kanisa la Kilutheri la KKKT linatumia jina "dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini kwa Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19 hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.

(The hood infotainment) Historia inasema kwamba asili ya Wanyakyusa ni mkoani Morogoro. Kabila hilo likitokana na kabila la Waluguru. Hili hasa ndilo chimbuko la Wanyakyusa.

Inasemekana kwamba mwindaji mmoja wa Kiluguru alitembea peke yake porini bila ya kuongozana na mtu mwingine. Alitembea hadi akafika maeneo ya Kabale huko Suma, Tukuyu wilayani Rungwe. Akiwa huko, akaendelea na kazi yake ya uwindaji.
Baadaye akatokea Mzulu mmoja kutoka Afrika Kusini aliyekuwa na binti yake. Akafika maeneo alikokuwa akiishi yule mwindaji Mluguru, naye akapiga kambi hapo Kabale, wakaungana katika maisha ya uwindaji.

Ikawa kila yule Mluguru akitoka asubuhi kwenda kuwinda, alikuwa akifanikiwa kurejea nyumbani na wanyama wakati rafiki yake wa Kizulu alikuwa akirudi mikono mitupu.

Kutokana na hali hiyo, Mluguru akageuka kuwa mfadhili wa Mzulu, kwa kutoa misaada mara kwa mara, na kwa kulipa fadhila hizo, akamwoza bintiye kwa Mluguru.

Akamwoa na maisha yakaendelea huku nyumbani kwa mwindaji wa Kiluguru na mkewe binti wa Kizulu, kukiwa hakukosekani nyama kama kitoweo.

Kwa sababu ili kuihifadhi nyama ilibidi kwanza ibanikwe, basi kitendo hicho kilisababisha harufu nzuri ya kitoweo kile kusambaa eneo kubwa na kufika hadi ukweni kwake nyumbani kwa Mzulu.

Ndipo Mzulu yule akawa anasema mara kwa mara: “Pale panatoa kyusi kila siku” akimaanisha moshi kwa lafudhi ya lugha ya kwao.

Mazoea ya kutamka ‘kyusi’ kila siku, yakaligeuza neno ‘kyusi’ na sasa likawa linatamkwa ‘kyusa’, baadaye ‘kyusa’ ilipozidi kutamkwa kwa mara nyingi, nayo pia ikabadilika bila kukusudia ndipo watu walipokuwa wakimwita Mluguru ‘Mnyakyusa’, kwa kuwa moshi ukiambatana na harufu ulikuwa ukitokea ndani ya nyumba yake na kusambaa.

Kwa hiyo, tangu hapo na kutokana na jina hilo alilopewa kwa ajili ya mazoea ya kukosea kutamka kitu, hata watoto wake pia waliozaliwa na Mluguru na mkewe Mzulu, wakawa wakiitwa ‘Wanyakyusa’.

Hiyo ndiyo asili na chimbuko la kabila la Wanyakyusa, na kwa kuwa Mnyakyusa alikuwa tayari ana asili ya pande mbili - wakati baba akiwa na asili ya Kiluguru na mama Mzulu wa ‘kwa Madiba’.

Na hata uchifu ukaanzia mahali pale palipokuwa panaitwa Kabale, na yule Mluguru aliupata uchifu kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwanzilishi na mkazi wa kwanza wa eneo lile na ndiye aliyekuwa anafahamika zaidi.

Mavazi yao

Kwa upande wa mavazi, Wanyakyusa walikuwa wakivaa mavazi yaliyokuwa yakijulikana kama ‘Lyabi’, Ni mavazi ya kwanza kwa kabila yakivaliwa enzi za utumwa. Mavazi haya ni yale yanayofunika maeneo ya siri pekee, na kwa wale ‘waheshimiwa’, kidogo basi wao walivaa vazi lililokuwa likiitwa ‘kikwembe’ au ‘kilundo’.

Mavazi haya yaliyovaliwa kwa mtindo kama lubega, ndiyo yaliyomtambulisha na kumtofautisha mhusika mbele ya jamii.

Ngoma yao

wanyakyusa wanangoma za aina nyingi kama
(a)MANG'OMA-hizi ni aina ngoma maarufu sana kwa wanyakyusa kama picha inavyoneka hapo chini,hizi ningoma zinazochezwa kipindi maalumu cha mwaka hasa baada ya mavuno,ngoma hizi ni maarufu kama MAPALANO,huchezwa sana ktk kipindi chajua.

(b) ;LUMOGHO-hu nimchezo unaochezwa kwa ustadi mkubwa sana wachezaji hutumia mikuki ambayo hurushwa juu na kutua chini,ngoma hizi huchezwa kwa umahili mkubwa sana kiasi chakuleta mvuto kwa watazamaji,ngoma hizi huonesha ushujaa nakujihami.

(c)MAGHOSI-hizi ni ngoma ambazo huchezwa hasa na vijana,mpiga ngoma huikalia ngoma nakupiga kwa mikono yote miwili,wachezaji hucheza na kuimba nyimbo nzuuri mfano kumsifia binti kwa uzuri wake natabia njema aliyonayo,ama kumkosoa kwa tabia yake mbaya,kwenye mchezo huu vijana wakiume nakike hujipamba nakufunga kanga/kitenge/shuka kiunoni ili aweze kukatika viuno vzr,kiukweri nimchezo wenye mvuto sana.

(d)MAPENENGA-huu pia nimchezo wangoma unaochezwa na jamii ya wazee jinsia zote,hizi ngoma huchezwa kwa madaha namaringo mengi,mchezo hueda taratibu sana lakini kwa mbwembwe na vituko vya hapa napale,

(e)SAMBA-huu pia ni aina ya mchezo unaotumia fimbo na vituko vingi,kifupi ngoma za kinyakyusa nikivutio kikubwa sana,waliobahatika kuona watakuwa mashuhuda.
hata ivo kuna mchezo unaitwa NGWAJHA-namingine mingi.

Chakula chao

Chakula chao kikuu na ambacho Mnyakyusa angeonekana kuwa amemkarimu mgeni, si kingine bali ni dizi zinazomenywa na kupikwa maarufu kama ‘mbalaga’.

Mnyakyusa halisi kama atakula chakula lakini akakosa ‘mbalaga’ hujiona kama bado hajakamilisha mlo, ingawaje siku hizi kuna mabadiliko fulani ambayo wengi hupendelea ugali na wali; lakini bado asili ya chakula chao hawawezi kuibadilisha kamwe.

Na ni lazima chakula kama ‘kande’ kipikwe kwenye tukio la msiba uwao wote, kama shughuli za msiba zitakwisha pasipo kupikwa chakula hicho chenye mchanganyiko wa mahindi na maharage; msiba huwa haujakamilika hata kama wafiwa ni watu wenye kujiweza kifedha zaidi lakini ni lazima kande zitapikwa japo kiasi.

Utamaduni wao
Kwa kawaida Wanyakyusa hawana mambo ya unyago kama ilivyo kwa baadhi ya makabila hapa nchini. Wao hawapendelei kabisa mila na desturi za kuwaweka mabinti ndani au kuwafanyia mambo yoyote ya tohara.

Hii ni pamoja na upande wa vijana wa kiume ambao nao hawafanyiwi ya tohara kama makabila mengine isipokuwa tu kwa upande wa vijana wa kiume mara tu wanapotimiza umri wa miaka 13 na kuendelea.

Hawa wazazi wao wa kiume huwatengea eneo ambalo kijana hutakiwa kujifunza kujitegemea akiwa bado mbichi. Hapo hutakiwa kuwa na kibanda chake na kuhama kutoka nyumba moja na wazazi wake



Sifa za Wanyakyusa wa Kyela

1. Wengi si wapole mtu afanyapo kosa
2. Wacha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau
5. Wanapenda kujulikana (hasa kama wamesoma hadi kupata digrii n.k.)
6. Wapiganaji sana kimaisha
7. Wana wivu katika masuala ya mapenzi
8. Wanapenda haki itendeke, hawapendi ubabaishaji
9. Ni watu shupavu sana kwenye kazi za kujitolea hasa za kijamii

Sifa za Wanyakyusa wa Tukuyu

1. Wapole
2. Wacha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau kabisa
5. Wanajituma kwenye kazi, hasa kilimo
6. Wana wivu sana
7. Wanapenda haki itendeke na hawapendi ubabaishaji
8. Ni watu jasiri na wasioogopa vitisho
9. Ni welevu

Chanzo: the hood info tainment na wikipedia



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

3 comments:

  1. ndugu yangu umetenda kosa kubwa la kushindwa kuwaelezea wanyakyusa japo sometimes unaingia kwenye ukweli mala unatoka tafadhali nakushauri utafute chanzo cha uhakika then uje uedit
    alafu Mnyakyusa hana wivu wa kila kitu moja kwa moja kama ulivyoandika nakuhakikishia ilo kwa sababu mim nmekaa na kulelewa na wanyakyusa huwa hawana wivu Myakyusa yupo tayari yeye aaibike ili amfurahishe mtu hapo ndo roho yake itakaa sawa

    alafu izo ulizoziandika ilikuwa ni mitazamo ya baadhi ya watu ni sawa na wewe leo utafute kabila ambalo halipo mtandaoni alafu uandike sifa zao kwa mtazamo wako unayowachukulia
    ila ungeniambia kubebana heeeeeeeeee akiwa rais Mnyakyusa mawazili woote hawatatoka mbali japo ni wachapa kazi na wana hofu ya MUNGU

    ila nmeipenda sana blog yenu hongereni sana asante

    ReplyDelete
  2. Ubaya uliopo hatuna huifadhi wa historia katika maandishi. Yatupasa tufahamu hata ibada ya kinyakyusa ilifanyikaje

    ReplyDelete
  3. Vizuri imesaidia zaidi kufahamu historia ya wanyakyusa.

    ReplyDelete

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts