Tuesday, 24 June 2014
TUKUMBUKE ENZI
Afrika ina makabila mengi ambayo hayawezi kuhesabika na vikundi vya kikabila na vya kijamii. Baadhi ya vikundi hivi vinaashiria wakazi wengi ambao ni mamilioni ya watu. Vikundi vingine ni vikundi vidogo vya watu elfu kadhaa.
Tanzania ina mila tajiri ya sanaa, sanaa za Tanzania hujieleza katika aina mbalimbali ya mchongo wa mbao, shaba na matendo ya sanaa ya ngozi. sanaa ya hii pia inajumuisha uchongaji, uchoraji, ufinyanzi, mavazi ya mwili na ya kichwa katika sherehe na mikutano ya kidini n.k
Tanzania ina mila tajiri ya sanaa, sanaa za Tanzania hujieleza katika aina mbalimbali ya mchongo wa mbao, shaba na matendo ya sanaa ya ngozi. sanaa ya hii pia inajumuisha uchongaji, uchoraji, ufinyanzi, mavazi ya mwili na ya kichwa katika sherehe na mikutano ya kidini n.k
kiasili mbeya ilikuwa eneo la wasafwa, siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa wasafwa pamoja na makabila ya wanyakyusa kutoka wilaya ya Rungwe na kyela, wanyiha kutoka mbozi, wandali kutoka ileje na wakinga kutoka makete. lakini kutokana na utandawazi na kuhama kwa watu kutokana na sababu mbalimbali hakika kwa sasa kila mkoa lazima ulikute kila kabila,
hadithi za mafuriko zilikuwa zikienea katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Kwa mfano kwa upande wa mbeya hadithi ya utokeaji wa ziwa kiungululu, kisiba, ikapu n.k inasemekana kwamba alitokea mtu mchafu aliyeomba maji katika nyumba kadhaa za jamii hizo na kunyimwa, lakini alikuwepo mama mmoja msamalia mwema alimtunza na kumpa chakula pamoja na maji. Mungu wake alimtuza kwa kumpa utajiri, alimshauri aondoke kutoka eneo hilo, na kuharibu jirani wake wachoyo. Baadhi ya mila na desturi zilizokuwa zimetawala katika jamii zetu ni pamoja na :-
Kumeza peke ya mchungwa.
Kulikuwa na imani kuwa ikatokea umemeza peke ya mchungwa basi mti utaota katika kichwa chako na wenzio watakuwa wanapanda mtini kuchuma machungwa, lilikuwa ni fundisho kubwa sana ambalo lilitufanya wengi tuwe makini pindi tulapo machungwa ama tunda loloto lenye peke. na ilikuwa kwa bahati mbaya ukameza basi nyumba nziwa watakuimbia nyimbo, watakusema na utakosa raha kipindi chote watakacho kusema.
Kukaa juu ya kinu kisha kuchafua hewa(kujamba).
Ilisemekana ukikaa juu ya kinu kisha ukachafua hewa basi utatokwa na majibu katika makalio yako, kinu kilitumika katika shughuri mbali mbali za jikoni hivyo haikuwa busara kukichafua, ndio maana wazazi wetu walitumia njia hiyo kutufanya tukiogope kinu.
Kuitika Usiku uitwapo na mtu usie mjua.
Ulikuwa huruhusiwi kuitika usiku pindi uitwapo na mtu usie mjua kwani ilisemekana unaitwa na jini hivyo utakapoitika basi utapotea na hutaonekana tena, Na masimulizi ya majini yalikuwa yakitisha sana katika jamii zetu kuwa majini huka watu hivyo ilikuwa ngumu sana kukaidi agizo hili.
Kuongea ukiwa chooni.
Wazee wetu walisema Ukiongea kama uko chooni basi utavimba mashavu, na hautokuja kupona kamwe, lakini maana yake ilikuwa tuwe wasafi maana chooni kuna mambo mengi sana.
je wewe pia ulipata kuyasikia haya? unaruhusiwa kucomment nasi tutafurahi sana kuona comment yako
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania
Ask a question
Archive
Popular Posts
-
Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI? Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyoto...
-
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini n...
-
J ami i ku b w a ku li k o j a m i i z ot e k a t i k a w i l a y a y a M b e y a n i W a s af w a . W asaf w a h uish i ...
-
Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri w...
-
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa . Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 1...
-
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, I...
-
Watu wa ndembo. moja kati ya wachezajia wa Ndembo akionesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki wake. wapiga ngoma wa nd...
-
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo. kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na...
-
Ni moja kati ya mimea ipatikanayo katika maeneo mbali mbali hususani katika mapori, mmea huu hutambaa kama mboga za maboga na ...
-
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani daki...
0 comments:
Post a Comment