Wednesday 25 June 2014

KIJUNGU JIKO.

kijungu jiko hupatikana katika mto kiwira maeneo ya KYIMO KIJIJI KITULIVU maarufu kama KK, eneo hili lipo wilaya ya Rungwe mkoani mbeya.

Haya ni maneno ya ukaribisho unayokutana nayo kabla hujaenda katika kijungu,

 Ukiwa juu kabla hujashuka katika usawa wa mto, utakiona kijungu kwa muonekano huu baada ya kusogea ndipo utaona vizuri sana.



mara baada ya kushuka hivi ndivyo mto kiwira huonekana kwa uzuri sana.

Hiki ndicho kijungu jiko na hapa ndivyo maji yanavyo ingia, ukiyatizama sana utaona kama yanachemka yakigonga chini.

Baada ya kuingia katika kijungu maji haya hutokeza upande huu kisha kuendelea na safari zake.


kwa mujibu wa mwenyeji wetu alisema mto huu hutiririsha maji yake kutoka mlima Rungwe mpaka ziwa Nyasa, maji ya mto huu yanapoingia katika kijungu yanaingia kwa kasi sana kisha kutokea upande wa pili yake, yakitoka huendelea na safari zake ambapo ni umbali mdogo kutoka eneo la kijungu mpaka lilipo daraja la mungu.

Kijungu jiko ni eneo lenye kustaajabisha sana kwa sababu kimeumbwa kwa mwamba na kufanya umbo la kama la chungu, ambacho hupokea maji yote ya mto huo na kuyapeleka chini bila kuyapitisha juu ya mwamba huo.

Inaelezwa kwamba ili mtu uvuke kwa usalama kwenye mwamba juu ya kijungu kutoka upande wa mashariki lazima atumie mguu mmoja wa kulia kisha kuusogega taratibu mpaka ukimaliza kuvuka, na ukitoka magharibi utatakiwa kutumia mguu wa kushotona kuusogeza taratibu huku mguu wa kulia ukifuata nyuma. kwa kufuata hayo hutatumbukia.

Kitu kingine ni uwepo wa imani kuwa endapo mtu akizama katika mto huo, lazima afuatwe mzamiajai aliyerithi kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo basi aliyezama atakaa katika shimo(mbako) kwa muda wa siku saba na muda huo ndugu mkiwa mtoni usiku na mchana ndipo atakuja kuonekana.

mwenyeji wetu hakuishia hapo alisema kwa mfano ukiwa na shilingi mia ukiirusha katika maji hayo, itakapo gonga maji itarudi na kuanguka pembezoni mwa mto huo na yale maji yaliyotwanyika yatajirudi na kupika katika mwamba ule na si nje ya mwamba.

Namna ya kufika, ukitokea mbeya au kyela unashuka KK kisha utaona kibao cha shule ya gods bridge na kimeonesha uelekeo, utafuata ule uelekea na utatangulia kuona njia panda yenye kuelekea daraja la mungu, ukinyoosha moja kwa moja utavuka eneo la  magereza na kufika kijungu jiko. ukiwa na gari binafsi pia inaweza kufika mpaka pale kipo kile kibao chenye maelezo ya malipo juu ya eneo husika. lakini ukienda daraja la mungu hakuna malipo yoyote.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.






0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts