Thursday, 23 October 2014

MAAJABU YA MUNGU RAMANI YA BARA LA AFRIKA ZIWA NGOSI

Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini na 33.553°Mashariki, ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya lile lililoko nchini Ethiopia. Hata hivyo, wataalamu wanasema kwamba Ziwa Ngosi lina sifa za kipekee linazolitofautisha na lile lililoko Ethiopia.

Moja ya tofauti hizo ni kwamba Ziwa Ngosi limezungukwa na milima na misitu minene tofauti na lile la Ethiopia ambalo liko eneo lililo wazi na hufikika kwa urahisi kabisa kwa gari kitu ambacho hakiwezekani kwa Ziwa Ngosi. Wataalamu wanasema kwamba kuwepo kwa ziwa hilo sehemu hiyo kunasaidia kuzuia milipuko ya mara kwa mara ya volkano kwa kuwa linasaidia kupunguza misukumo ya gesi inayojijenga chini na kuanza kutafuta upenyo wa kutokea chini ya ziwa. Kitu cha kushangaza ni muonekano wa ziwa hili linakaribia kuwa na muonekano kama ramani ya bara la afrika pamoja na visiwa vyake kama ilivyo kule njombe ambapo kuna mwamba wenye ramani ya bara la Afrika unaitwa Lwivala, uliopo katika pori la hifadhi ya msitu Lwivala kijiji cha Igodivaha Wilaya ya Njombe

ziwa hili pia lina ingiza tu maji na hali toi maji kwa sababu liko katikati ya milima hivyo kuonekana kama liko shimoni alafu halina ufukwe, ziwa hili linalopatikana katika Hifadhi ya msitu Uporoto (Poroto Ridge) yenye eneo la hekta 9,332 ipatikanayo karibu na vijiji vya Kisanga 4.3km Uyole (24.4km) na mji mdogo wa Tukuyu upatikanayo wilaya ya Rugwe. Zipo imani nyingi potofu juu ya ziwa hilo la maajabu watu husema ziwa hili lilichomwa moto na wakazi wa kijiji cha Mwakaleli kwasababu lilikuwa likileta mikosi mingi kijijini hapo ikiwemo vifo vya mara kwa mara kitu ambacho si sahihi kitaalam ziwa haliwezi kuhama, Zipo imani miongoni mwa watu kuwa ziwa ngosi watu wanapotea kimazingara, kuwapo kwa sauti za watu wasioonekana ndani ya misitu, wengine husema ziwa hilo limekuwa likigeuka rangi mara kwa mara na kuwa na rangi za kijani, bluu, nyeusi na nyeupe kitu ambacho kinawafanya waamini kuwa ziwa hilo sio la kawaida.

Chief mkuu wa wasafwa mkoa wa mbeya Chifu Rocket Masoko Mwanshinga alisema ni jambo la ajabu na kusikitisha sana kuona ziwa ngosi linafahamika sana kwa wageni kuliko wenyeji, hivyo anapenda kutoa wito kwa wadau wote wa utalii kulitangaza ziwa hili ili liweze kufahamika sana ndani na nje ya nchi. alisema jina hilo ni la kisafwa linalotokana na neno Gosi lenye maana ya kubwa hivyo kwa wasafwa walimaanisha ziwa kubwa na pia alisema maji ya ziwa lile ni maji safi na ya baraka tofauti na vile watu wanaamini.

Safari ilijumuisha washiriki 30 kutoka taasisi mbalimbali kama Mbeya Living Lab, FRESOWE, Mbeya Home of Tourism Blog, Mbeya Youth Development Network (Vijana Mbeya) na EGY business solution na watu binafsi ambao kwa ujumla ilikamilisha idadi hiyo ya watu 30.

Safari ilianza eneo la Uyole ya kati Kibao cha Coca Cola mnamo saa 2:00 asubuhi kuelekea ziwani ambapo washiriki karibu wote walikua wamewasili tayari kwa safari tukiwa tunaongozwa na kiongozi mteule kutoka Tanzania Forest Servises (TFS) ajulikanae kwa jina la Mr. Manaseh

Katika safari yetu ilitubidi kugawa makundi mawili ya watu 15 ili kurahisisha kutambuana ambapo kundi namba moja (1) lilikuwa chini ya modesto winfred na kundi namba mbili(2) lilikuwa chini ya amos asajile, hivyo washiriki wote tulifika kituo cha kwanza mnamo saa 4:30 Na kupumzika kwa muda wa dakika 20, ndipo tulipoanza safari kueleke kituo cha pili ambapo ilikuwa ndio sehemu ya juu ya milima inayolizunguka ziwa ngosi tulipumzika na kupata chakula cha mchana, mahali hapa palikuwa na upepo mwanana na baridi kali sana iliyopelekea watu wote kuvaa tena masweta yetu.

Hatukuishia hapo ndipo safari ikaanza tena na hapa ndipo kindumbwe ndumbwe kikaanza kwani ilikuwa sehemu ngumu sana ambayo ikapelekea idadi kubwa ya watu kushuka kwa kutumia makalio, baada ya kumaliza kile kilima ndipo moja kwa moja tukaingia katika ule msitu mnene mithili ya Amazon kutokana na kukosekana kwa alama zenye kuonyesha muelekeo kundi namba mbili (2)  tukapotea na kujikuta tukielekea usawa wa afrika kusini badara ya kwenda ule upande viliko visiwa. Na kibaya zaidi ni kwamba Muwapo ndani ya msitu huo hakuna simu inayoshika kutokana na kukosekana kwa mtandao hivyo ikawa ngumu kuwasiliana na kundi namba (1)  lakini tulipofika mbele tukakuta njia haionyeshi kuwa kuna watu wamepita hivyo tukarudi nyuma na kuikuta njia ambayo wenzetu walipita hivyo kundi namba moja waliwahi kufika lakini kundi namba mbili tukachelewa kidogo kufika.

Kutokana na maelezo tuliyokuwa tumepewa na Tanzania forest services nyanda za juu kusini ilikuwa ngumu kuwaruhusu watu kuogelea hivyo hakuna mdau yeyote aliyeogelea ziwani hapo kwa sababu za kiusalama. Tukapumzika kidogo na kisha tukaanza ratiba ya michezo na matukio mbali mbali kama yalivyokuwa yameandaliwa kama vile kutaja vivutio vipatikanavyo maeneo ya mkoa wa Mbeya (Naijua Mbeya Kuliko wewe), kukimbia na yai katika kijiko na shindano la hisia (kulia) ambapo washindi waliopatikana walikabidhiwa zawadi zao kutoka kwa taasisi wadhamini wa mashindano hayo, mara baada ya kumaliza hayo ndipo saa 9 jioni tukaanza safari ya kurudi kwa makundi kama awali.

Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyekuwa pamoja nasi katika safari yetu kwani wote tulikwenda salama na kurudi salama hakuna hata aliyeumia katika safari hii. Pia tupende kutoa shukrani zetu za dhati kwa taasisi wasiriki, kamati ya utalii ya mkoa wa mbeya na wadau wote walioshiriki ambao kiukweli kutokana na wingi wao itakuwa ngumu kuwataja kwa majina.

Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinakwamisha sana kukua ama kufahamika kwa ziwa ngosi miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na, Miundo mbinu mibovu ambayo hupelekea watalii kushindwa kufika kwa urahisi katika eneo husika, Viongozi wachache wa safari (tour guides), Matangazo ya kivutio, Taarifa na maelezo hafifu ya kivutio, Makosa ya matamshi ya jina. Pamoja na hayo Jitihada muhimu zinahitajika ikiwemo kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababisha udongo kuingia ziwani hivyo kupunguza kina cha ziwa, kujenga angalau ngazi zenye sehemu za kujishikiria katika baadhi ya maeneo ambayo ni tatanishi/magumu kupanda ama kushuka, vyombo mbali mbali vya habari kujitokeza kwa wingi kulitangaza ziwa ngosi, pia kujenga kijisehemu kidogo ambacho kitatoa huduma muhimu ikiwemo chakula na vinywaji.

 Muonekano wa ziwa ngosi muwapo sehemu ya  juu ya milima iliyolizunguka ziwa hilo

Jiwe linalopatikana njombe lenye muonekano wa ramani ya bara la afrika

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya

5 comments:

  1. Asante kwa taarifa nzuri Amoc
    nilifika hapo mwaka 1999 nikiwa kidato cha tatu Mbeya day!
    katika story yako hujaeleza kama mlifanikiwa kuogelea ndani ya ziwa hilo la maajabu naweza kusema.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kutokana na sababu za kiusalama ilikuwa ngumu sana kwetu kuogelea japo tuliweza kuyagusa maji kwa namna moja na nyingine

      Delete
    2. kuna viumbe hai ndani ya ziwa hiloo ?

      Delete
  2. TunaweZa kutembelea na cc tukaliona hlo zwa

    ReplyDelete
  3. kuna viube hai ndani ya ziwa hilo?

    ReplyDelete

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts