Monday, 30 June 2014

UNAFAHAMU NI KWA NINI SAFU HIZI HUITWA SAFU ZA MILIMA LIVINGSTONE?

Picha ya safu za milima livingstone ukiwa maeneo ya Lufilyo halmashauri ya Busokelo, wilaya ya Rungwe.

Livingstone alitafuta njia ya usafiri kati ya eneo la Watswana na pwani la magharibi ya Afrika hivyo akaanza safari kubwa iliyompeleka hadi Luanda(Angola). Aliporudi alikuwa Mzungu wa kwanza wa kuona maporomoko ya Victoria Falls mwaka 1855. Mwaka uliofuata alifika Msumbiji alipokuta meli iliyompeleka Uingereza.

Livingstone alipokelewa kama mshujaa kwa sababu taarifa zake zilisababisha kuchorwa upya kwa ramani za Afrika. Alipata sifa nyingi kama mtaalamu wa jiografia na mpelelezi. Kitabu chake "Missionary travels and researches in South Africa" ilisifiwa kote. Serikali ya Uingereza alimpa cheo cha konsuli katika Msumbiji akarudi Afrika. Sasa alijaribu kufuata mwendo wa mto Zambezi kutoka mdomo wake akafika kwenye mto Shire na Ziwa Nyasa (Malawi). Safari zilizofuata 1866 zikampeleka hadi ziwa Tanganyika. 1870 alielekea magharibi kutoka Ujiji akafikia mto Lualaba katika Kongo. Aliporudi Ujiji alikutana na Mwamerika Henry Morton Stanley aliyeongoza msafara wa kumwokoa Livingston lakini hali halisi Stanley alihitaji msaada na Livongstone aliweza kumsaidia kupitia marafiki zake wazalendo.

Safari yake ya mwisho ililenga kugundua chanzo cha mto Nile. Hapo Livingstone aliaga dunia mnamo tar. 30 Aprili 1873 katika kijiji cha Chitambo (Zambia). Watumishi wake chini ya uongozi wa Myao Susi walizika moyo wake palepale wakakausha maiti yake wakaibeba hadi Bagamoyo iliposafirishwa kwa meli Uingereza na kuzikwa London katika kanisa la Westminster Abbey tar. 18 Aprili 1874.

Hadi leo kumbukumbu ya Dr. David Livingstone inaheshimiwa mahali pengi pa Afrika. Mahali pafuatapo paitwa kwa jina lake:
·         Milima ya Livingstone katika Tanzania upande wa mashariki ya Ziwa Nyasa
·         Mji wa Livingstonia katika Malawi
·         Mji wa Livingstone katika Zambia
·         Kisiwa cha Livingstone katikati ya maporomoko ya Victoria Falls
·         Maporomoko ya Livingstone Falls ya mto Kongo
·         Mji wa Blantyre (Malawi) umepewa jina lake kutokana na mji Blantyre katika Uskoti alikozaliwa Livingstone.
Chanzo: Wikipedia.



  KARIBU TANZANIA, KARIBU MBEYA.


0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts