Sunday, 22 June 2014
KIMONDO CHA MBOZI.
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 12, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya, Tanzania.
Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.
Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8,69%, sulfuri0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Kina muonekano mithiri ya jiwe lakini ajabu yake ni pale utakapo kigonga kinatoa mlio kama wa debe tupu.
Muonekano wa kimondo hicho kilichopo mkoani mbeya, katika wilaya ya mbozi.
jiwe hili la chuma kwa ukaribu huonekana hivi.
hapo ni kama kachungu kana maji ukiyagusa ni ya baridi sana kama yametoka katika jokofu
Eneo hili wataalam wa mambo ya jiolojia walikata kipande cha jiwe la chuma hicho ili kufanyiwa utafiti.
Kimondo hiki kipo umbali wa kiasi cha kilometa 70 kutoka Mbeya mjini, kusini mwa Tanzania, katika barabara kuu ya Tanzania-Zambia, njia kuu ya kwenda Tunduma.
Hakuna anayejua kimondo hicho kilianguka lini, lakini lazima iwe kilianguka zamani sana kwani hakuna hekaya zozote kukihusu. W. H. Nott, soroveya kutoka Johannesburg, aliandika kwamba aliona kimondo hicho mnamo Oktoba 1930. Tangu wakati huo, mtaro ulichimbwa kukizunguka, na kufanya kionekane kana kwamba kimeinuliwa na kuwekwa juu ya madhabahu ya mawe. Hivyo, kimondo hicho kimebaki mahali kilipoanguka.
Watu fulani wamejaribu kukata sehemu fulani ya kimondo hicho ili kujiwekea kama kumbukumbu, lakini hiyo ni kazi ngumu sana. Mnamo Desemba 1930, Dakt. D. R. Grantham wa Chama cha Jiolojia alipojaribu kukata kisehemu cha karibu sentimeta kumi kwa msumeno, ilimchukua muda wa saa kumi! Kisehemu hicho kinaweza kuonekana katika mkusanyo wa vimondo kwenye Jumba la Makumbusho la Uingereza huko London.
Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya
Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania
Ask a question
Archive
Popular Posts
-
Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI? Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyoto...
-
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini n...
-
J ami i ku b w a ku li k o j a m i i z ot e k a t i k a w i l a y a y a M b e y a n i W a s af w a . W asaf w a h uish i ...
-
Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri w...
-
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa . Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 1...
-
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, I...
-
Watu wa ndembo. moja kati ya wachezajia wa Ndembo akionesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki wake. wapiga ngoma wa nd...
-
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo. kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na...
-
Ni moja kati ya mimea ipatikanayo katika maeneo mbali mbali hususani katika mapori, mmea huu hutambaa kama mboga za maboga na ...
-
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani daki...
0 comments:
Post a Comment