Sunday, 7 September 2014
SAFARI YA KUPANDA MLIMA LOLEZA KUTOKA MWANZO HADI KITUO CHA 15
Kushoto ni Mkurugenzi wa FRESOWE Tanzania, Miraji Ngwata , na Modesto Winfred wakiwa Round about iliyopo katikati ya jiji la Mbeya, wakiwasubiri washiriki wengine kutoka maneneo mbali mbali ya jiji tayari kwa maandamano.
Walioshika bango ni wawakilishi wa Mbeya youth development network (Vijana Mbeya) kushoto ni Kelvin Paul (publi realtion officer) na kulia ni Steve Mwakakeke Katibu mkuu wa vijana Mbeya, na hapa tuko RETCO tulipoanzia maandamano kisha kuelekea njia ya hospitali ya Rufaa ielekeyo mlimani.
kushoto ni Amos Asajile,Tabitha Bugali, Steve Mwakakeke na Kelvin Paul Tukimuaga bibi yetu baaada ya kutusundikiza kutoka RETCO hadi mwanzo wa mlima Rufaa kwa juu kidogo.
Mdogo mdogo safari ikaanza, vijana wakiwa wenye nguvu na furaha tele
Mkurugenzi wa FRESOWE akimuonesha dada nyoka aliekuwa kajiviringa juu ya mti.
Mdogo mdogo safari ikaanza, vijana wakiwa wenye nguvu na furaha tele
Mkurugenzi wa FRESOWE akimuonesha dada nyoka aliekuwa kajiviringa juu ya mti.
Hawakuficha furaha zao, katikati ni mkurugenzi wa T Motion bwana Robert Elia
washiriki wakionesha furaha zao kwa mapozi mbali mbali katika picha.
Mama yetu ambae hakutaka kutuacha peke yetu, alitusindikiza mpaka juu ya mlima ambae pia ni Mwenyekiti wa YWCA Oliver Kibona akiwa na mwandishi wa habari katika kituo cha BARAKA FM dada Ikupa Mwasumbi.
Mara baada ya kupata maneno machache kutoka kwa mama Bugali, tukaanza safari yetu saa 2:23 na kufika katika kituo cha 15 saa 3:23 asubuhi.
Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Wednesday, 3 September 2014
MAANDALIZI YANAZIDI KUPAMBA MOTO
Tshert itakayovaliwa siku ya jumamosi ya tarehe 06/09/2014 upande wa nyuma itasomeka NITASIMAMA, NITATEMBEA KIZAZI KIPYA CHA VIJANA UTHEBUTU UNAANZIA NYUMBANI.
Upande wa mbele wa tshert itasomeka MBEYA YOUTH EVENT 2014,
Vuvuzela ndogo zitakazo pigwa baada ya kufika juu kileleni ikiwa kama ishara ya furaha baada ya vijana wa jiji kuwa pamoja katika Mlima Loleza
Hapa ni baadhi ya bendera zitakazoshikwa na washiriki wote watakao shiriki kupanda mlima, zipo za kutosha kiasi kwamba hakuna atakae kosa..
MTUSAMEHE KWA KUCHELEWE KUTOA TAARIFA
KUHUSU T-SHIRT, kuhusiana na event ya kupanda MLIMA LOLEZA, siku tayari
zimeisha kwa ambaye utahitaji uwe na t-shirt yenye ujumbe huu wa event,
unaweza ukatuagizia ili tukutengenezee au ukatuletea T-SHIRT NYEUSI yakwako au ukatuma
fedha ili ukatafutiwe t-shirt na upatiwe kabla ya ijumaa saa kumi
jioni, gharama ukituletea t-shirt utaambatanisha ba Tsh 3000, na unaweza ukatuagiza
tukutafutie ya aina gani, MTUSAMEHE KWA KUCHELEWESHA KUWAJULISHA,
jumamosi hii haitakuwa ya kusahaulika , mawasiliano zaidi 0764761900 ,
na 0715850113. ukishindwa kuipata usiwaze kushiriki ni haki yako kwa
mliotupa majina tayari MUNGU AWABARIKI
Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
WAJIBIKA ENVIRONMENT CLUB 1,YAFUNGULIWA MBEYA KATIKA SHULE YA MAPINDUZI
WAJIBIKA mpango huu unajulikana kama harakati za vijana katika uwajibikaji kiuchumi na kimazingira ili kuleta maendeleo endelevu, mradi huu unaosimamiwa na YWCA TANZANIA,YWCA MBEYA kwa ufadhili wa Y GLOBAL KFUK ambao umelenga katika humasisha vijana kuwa na uthubutu katika mambo mbalimbali,
WAJIBIKA CLUB 1,hili ndilo jina la club katika shule ya msingi mapinduzi iliyo katika jiji la mbeya ambapo mradi wa wajibika utakuwa ukifanya kazi hapo shuleni
wanaclub ya mazingira wakijadiri mambo mbalimbali
mwandishi wa habari na mkufunzi wa mazingira FESTO SIKAGONAMO akisisitiza jambo
walimu na wanafunzi wote katika kujifunza kufahamu kuhusiana na MAZINGIRA,
viongozi wa WAJIBIKA CLUB 1
DEBORA NJULUMI(program officer) akiwa na wanachama wa club
shughuli ndiyo kwanza imeanza vijana wana moyo wa kujitolea na kufanya kazi, mazingira ni yetu sote
Chanzo: www.ywcambeya.blogspot.com
Sunday, 31 August 2014
SHEREHE YA MATAMBIKO KABILA LA WASAFWA, MSITU WA IGANJO
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo.
kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na katikati ni Chifu Rocket Mwanshinga na wasaidizi wake.
Mh. Joseph Mbilinyi (mbunge wa Jiji la Mbeya) na Chifu wakipiga picha ya pamoja
Picha ya pamoja ya chifu, wasaidizi wake na wageni waalikwa
Njuga zinazotumika kuchezea ngoma; huvaliwa miguuni ambazo husaidia sana kuleta radha ya ngoma.
Wakina mama wakicheza ngoma ijulikanayo kwa jina la Mbeta
Wanaume wakicheza Mbeta,
Ishara ya kidoogo inayotumiwa na hao mapacha, ikimaanisha "kukumbukwa angalau kidogo" hasa ikiwalenga viongozi
mapacha wakiwa na Mh. Joseph Mbilinyi, na muwakilishi wa mbeya home of tourism modesto
- kuwakumbuka ndugu waliokufa
- matambiko kama kuomba mvua, amani uchaguzi, magojwa biashara na mengine
- sherehe inayohusisha wasafwa wote na wageni waalikwa kufurahi kwa pamoja.
- hotuba ya chifu
Sherehe hio huongozwa na chifu (mwene) wa kisafwa anaetambulika kwa jina la Mwene Rocketi Mwanshinga ambaye ndio chifu mkuu wa wasafwa wote. chifu huyu alisema tangu apate uchifu huo hajawahi kunyoa nywele
Pia sherehe hiyo hufanyika katika msitu uitwao Iganjo upatikanao maeneo ya Uyole Igawilo. Msitu huo unalindwa kijadi na unamaajabu mengi sana kuna sehemu ambazo huruhusiwi kupiga picha kwa sababu ya taratibu za msitu huo.
Wageni mbalimbali huarikwa katika sherehe hizo bila kujali kabila wala dini.
Karibu Tanzania karibu Mbeya.
MAJI MOTO KILAMBO.
Nlipofika eneo hili nikajaribu kuweka vidole katika maji na nkakuta ni ya moto kiasi kwamba huwezi kuvumilia kuweka vidole ndani ya maji yale kwa muda mrefu.
Haka ni kashimo kadogo lakini ukiangalia maji yake yanatokota kama maji yaliyochemka kwa mda mrefu motoni.
Hii ni chem chem inayorusha maji nayo ni ya moto sana.
Ukiangalia vizuri maji haya kama pana mvuke, ni kutokana na kuwa ya moto hivyo yanatoa mvuke.
Kwa mbali ni muonekano wa eneo la maji moto.
Maji moto haya yanapatikana katika Halmashauri ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe katika eneo maarufu kwa jina la Kilambo lakini ni kijiji cha ikapu ambacho kimepakana na Mbambo. Kilambo ni neno la kinyakyusa lenye maana ya Magadi.
Maji haya ukiyanywa yana radha ya chumvi kitu ambacho kimepelekea sehemu kubwa ya wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani kwenda kunywesha ng'ombe zao maji, Tulikutana na watu kutoka makete, lusungo, lufilyo, mbigili, ikama, mbande, busoka, kasyabone wakiwa na ng'ombe zao. jambo la ajabu ni kwamba mifugo hiyo ikikaribia kufika maeneo hayo hukimbia na huongoza yenyewe kuelekea hapo Muda mwingine wanadai ng'ombe huweza kutoroka zizini ili wakanywe maji yale.
Sehemu hii inavijisehemu vitano, ambapo sehemu za mwanzo maji chumvi yake si kali sana lakini sehemu ya mwisho ni kali sana na ndipo hapo mifugo mingi hupendelea kunywa, Katika chanzo maji ni ya moto yenye uwezo wa kuchemsha yai kwa muda mfupi sana yakishuka kidogo yanakuwa ya vuguvugu na yakiungana na mto uliopita eneo hilo huwa yabaridi kabisa.
Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Saturday, 30 August 2014
NAIJUA MBEYA KULIKO WEWE
Mtandao wetu unatambua umuhimu/ mchango wa kila mwananchi katika kukuza utalii wa mkoa wa Mbeya, hivyo umeandaa programu itakayo kwenda kwa jina la NAIJUA MBEYA KULIKO WEWE, Mimi kwanza.
Mtandao huu unatoa nafasi kwa mtu yeyote kutuma picha za kivutio chochote cha kitalii katika mkoa wa mbeya alicho tembelea katika barua pepe mbeyahomeoftourism2@gmail.com au inbox ya facebook page yetu.
Picha zitakazo tumwa ziambatane na taarifa muhimu kama vile wapi mhusika alitembelea na alipenda nini katika maeneo hayo na je nini ushauri wako juu ya sehemu uliyotembelea. kisha mtandao huu utazirusha katika blog yetu na facebook page yetu.
Jivunie Kuwa wa kwanza kuijua mbeya kuliko mwingine yeyote, Sema mimi kwanza.....!!
Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
SEMINA YA KUJALI MTEJA ILIYOANDALIWA NA MRADI WA SPANEST.
Mratibu wa mradi wa SPANEST Godwell Ole Meing'ataki akimkaribisha mgeni rasmi
Picha ya pamoja, kulia ni mratibu wa mradi wa SPANEST katikati mgeni rasmi na kushoto Mkufunzi Gosbert Kakiziba
mgeni rasmi akichukua kifungua kinywa
Mkufunzi Gosbert Kakiziba akiwa anafundisha
baadhi ya washiriki wakisiliza semina
mwakilishi wetu Modesto Winfred akiwa katika semina
Jackline na Getrude wakipata maelezo juu ya mbeya home of tourism kutoka kwa modesto mara baada ya chakula.
Semina ya KUJALI MTEJA (Customer care) iliyoandaliwa na mradi wa SPANEST(
Strengthening Protected Areas Network in Southern Tanzania) kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa mbeya iliyofanyika siku mbili tarehe 26 na 27/08/2014 katika ukumbi wa Mtenda Sun Set Hotel iliyopo Soweto Mbeya.
Katika semina hii tuliweza kujifunza mambo mengi katika maada nne (4) ambazo ni :-
- Huduma kwa njia ya mawasiliano
- Kujali Saikolojia ya mteja
- Kujenga Uhusiano na
- Wateja na Kujali wateja na kutawala Hisia zao.
Mafunzo haya yalihudhuriwa na taasisi za kiserikali na zile za binafsi lengo kuu ikiwa ni kuwezesha washiriki kukuza uwezo wa kutoa huduma zitakazo wezesha mkoa wa Mbeya kukua kiuchumi, pia kuufanya mkoa wa Mbeya kuwa kitovu cha uchumi, kukua katika sekta ya utalii, chaguo la kwanza kwa uwekezaji, chanzo cha ajira, na kitovu cha weredi na ukarimu katika kutoa huduma.
Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania
Ask a question
Archive
Popular Posts
-
Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI? Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyoto...
-
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini n...
-
J ami i ku b w a ku li k o j a m i i z ot e k a t i k a w i l a y a y a M b e y a n i W a s af w a . W asaf w a h uish i ...
-
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, I...
-
Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri w...
-
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa . Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 1...
-
Watu wa ndembo. moja kati ya wachezajia wa Ndembo akionesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki wake. wapiga ngoma wa nd...
-
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo. kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na...
-
Ni moja kati ya mimea ipatikanayo katika maeneo mbali mbali hususani katika mapori, mmea huu hutambaa kama mboga za maboga na ...
-
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani daki...


























