Sunday 7 September 2014

SAFARI YA KUPANDA MLIMA LOLEZA KUTOKA MWANZO HADI KITUO CHA 15

 Kushoto ni Mkurugenzi wa FRESOWE Tanzania, Miraji Ngwata , na Modesto Winfred wakiwa Round about iliyopo katikati ya jiji la Mbeya, wakiwasubiri washiriki wengine kutoka maneneo mbali mbali ya jiji tayari kwa maandamano.

 Walioshika bango ni wawakilishi wa Mbeya youth development network (Vijana Mbeya) kushoto ni Kelvin Paul (publi realtion officer) na kulia ni Steve Mwakakeke Katibu mkuu wa vijana Mbeya, na hapa tuko RETCO tulipoanzia maandamano kisha kuelekea njia ya hospitali ya Rufaa ielekeyo mlimani.

kushoto ni Amos Asajile,Tabitha Bugali, Steve Mwakakeke na Kelvin Paul Tukimuaga bibi yetu baaada ya kutusundikiza kutoka RETCO hadi mwanzo wa mlima Rufaa kwa juu kidogo.

 Mdogo mdogo safari ikaanza, vijana wakiwa wenye nguvu na furaha tele

 Mkurugenzi wa FRESOWE akimuonesha dada nyoka aliekuwa kajiviringa juu ya mti.

 Hawakuficha furaha zao, katikati ni mkurugenzi wa T Motion bwana Robert Elia

 Vijana wa vuvuzela wakizipiga kwa shangwe wakiongozwa na Emanuel Mwansasu baada ya kufika kituo cha 15 safari ambayo ilikuwa ngumu sana,

washiriki wakionesha furaha zao kwa mapozi mbali mbali katika picha.

Mama yetu ambae hakutaka kutuacha peke yetu, alitusindikiza mpaka juu ya mlima ambae pia ni Mwenyekiti wa YWCA Oliver Kibona akiwa na mwandishi wa habari katika kituo cha BARAKA FM dada Ikupa Mwasumbi.

Tulipofika katika kituo cha 15 ambayo ni karibu nusu ya safari, tukapata chochote kitu kilichokuwa kimeandaliwa na waandaaji wa safari hii.

Kwakuwa moja ya madhumuni yetu ilikuwa kutunza mazingira, baada ya kula tukakusanya makaratasi yote na kuyaweka sehemu moja,kisha safari ikaendelea.

Mara baada ya kupata maneno machache kutoka kwa mama Bugali, tukaanza safari yetu saa 2:23 na kufika katika kituo cha 15 saa 3:23 asubuhi.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts