Sunday, 7 September 2014
MLIMA LOLEZA WAPAMBWA
Safari ikaaza na hapa ni sehemu maarufu kama mlima kucha, ni sehemu ambayo kupanda kwake hata uwe mbishi kiasi gani lazima utapandia mikono,
Kulia ni Mtu wa kwanza kufika kileleni katika jopo la watu sabini na tisa (79) Mr. Michael Peter (meek mil)
Omary Mwakipesile aliekuwa wa pili kufika katika kilele cha mlima loleza katika facebook ni maarufu kama Swaiba Mswahili.
Katibu wa mbeya youth develoment network akiwa na elly bonke wakizungumza na mshindi wa shindano la kula upande wa wasichana lililojumuisha washiriki saba (7)
Mshindi wa pili Venance Shitindi katika shindano la SIJAWAHI ONA lililokuwa limedhaminiwa na mbeya home of tourism, alisema hajawahi ona mwanafunzi wa kidato cha pili hajui bara lake. Lakini mshindi wa kwanza alisema hajawahi ona kondakta au mpiga debe wa ndege, na hapa ni mr Modesto kutoka mbeya home of tourism akimkabidhi zawadi yake, ambapo mshindi wa kwanza alijinyakulia Tshert na mshindi wa pili alijinyakulia pesa.
Igizo lililoigizwa na vijana (7)ambalo lilimhusu kijana aliesoma kwa shida sana na kubahatika kumaliza elimu ya chuo, kutokana na uhaba wa ajira akajiingiza katika biashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya, anakamatwa na polisi na mwisho wake ukawa kuozea gerezani.
Neno la mwisho kutoka kwa vijana ni TUMETHUBUTU,
Mshindi wa kwanza wa mbio akikabidhiwa zawadi yake kutoka kwa waandaaji wa shindano hilo. alikimbia kwa muda wa dakika 44:42, mshindi wa pili elly bonke alikimbia kwa dakika 45:31 na mshindi wa tatu alikwenda kwa dakika 45:59
Kama ilivyokuwa shida kupanda hali kadharika kushuka pia ikawa zaidi ya shida, kupanda ni lazima upandie mikono basi katika kushuka style inabadirika ni lazima makalio yatagusa chini.
Baada ya kushuka baadhi ya washiriki wakapiga picha ya pamoja na wengine wakawa tayari wametangulia majumbani kwao.
Matukio kadhaa yaliweza kuipamba siku yetu tulipokuwa mlimani, kulikuwa na nyimbo zilizoibwa kwa lugha tofauti, mashindano ya kula kwa wavulana na wasichana, kulikuwa na igizo, na mashindano ya mbio.safari yetu ilikuwa ni ya watu 79 amabo wote waliweza kupanda na hatimae kushuka salama.
Awali ya yote tupende kutanguliza shukrani za dhati kwa Taasisi zote na wale wote walioshiriki katika tukio hili la kupanda mlima loleza, kiukweli tumejifunza mengi kutoka kwa kila mmoja kama mlivyoweza kubadirishana mawazo na kutengeneza familia moja ambayo tunaamini tutashirikiana sana katika kila jambo la maendeleo.
Tupende kutambua mchango mkubwa uliooneshwa na kituo cha radio BARAKA FM 107.6 MHz sauti ya matumaini na ukombozi, ambao walitambua umuhimu wa event hii katika mkoa wetu, hivyo kujumuika nasi mwanzo mpaka mwisho wa tukio hili, pia waliweza kurusha matangazo live kutoka mlima loleza na kuzungumza na baadhi ya washiriki.Tulianza kushuka saa 8:42 na kufika katika kituo cha 15 saa 9:21 na tukaondoka hapo saa 9:29 na kufika chini saa 10:00 jioni.
kwa mawasiliano juu ya ushauri au chochote tutumie katika email: mbeyayouthevent2014@gmail.com na simu: ELLY BONKE 0764761900
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania
Ask a question
Archive
Popular Posts
-
Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI? Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyoto...
-
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini n...
-
J ami i ku b w a ku li k o j a m i i z ot e k a t i k a w i l a y a y a M b e y a n i W a s af w a . W asaf w a h uish i ...
-
Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri w...
-
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa . Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 1...
-
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, I...
-
Watu wa ndembo. moja kati ya wachezajia wa Ndembo akionesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki wake. wapiga ngoma wa nd...
-
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo. kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na...
-
Ni moja kati ya mimea ipatikanayo katika maeneo mbali mbali hususani katika mapori, mmea huu hutambaa kama mboga za maboga na ...
-
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani daki...
0 comments:
Post a Comment