Wednesday, 17 September 2014

CHIEF MKUU WA MBEYA AZUNGUMZIA SAFARI YA ZIWA NGOSI

 
Kutakuwa na michezo ifuatayo 1. Mchezo wa hisia (kutoa machozi) Mchezo huu utakua na washiriki nane (8) ambao watachukua namba za ushiriki kuanzia101-108. Mdhamini wa mchezo huu atakua ni FRESOWE 2. Kuziba macho nakutembea katika vibox Mchezo huu utakua na washiriki nane (8) ambao watachukua namba za ushiriki kuanzia 109-116. Mdhamini wa mchezo huu ni EGGYBUSINESSSOLUTION.BLOGSPOT.COM  3. Kutembea na yai juu ya kijiko Mchezo huu utakua na washiriki sita (6) ambao watachukua namba za ushiriki kuanzia 117-122. Mdhamini wa mchezo huu ni MBEYA LIVING LAB.  4. Kutaja vivutio visivyo julikana (naujua Mbeya kuliko wewe)  Mchezo huu utakua na washoriki kumi (10) ambao watachukua namba za ushiriki kuanzia 123-132. Mdhamini wa mchezo huu ni MBEYA HOME OF TOURISM.

Muda mchache uliopita tukafunga safari na kuelekea nyumbani kwa Chief mkuu wa wasafwa mkoa wa Mbeya Chief Mwanshinga ili kuweza kupata maelezo ya Ziwa Ngosi kwa undani kabla ya safari, alisema Ziwa hili ni la Mungu hivyo liko salama japo watu wake hulipamba kwa namna wanavyujua wao, Japo alitusihi sana tusiende na kuogelea katika ziwa lile. aliongea mengi sana ya kututia moyo na kuondokana na mila potofu zinazosemwa na wengi zaidi akasema niwatakie safari njema yenye heri na mafanikio tele.

Washiriki wote waliojipanga katika mashindano mbali mbali yatakayo kuwepo watakuwa na namba maalum za ushiriki ili waweze kutambuliwa kiurahisi, tunawaomba wote mliojiandaa kushiriki mjiandae vyema maana taasisi zilizodhamini pia zimejiandaa vyema kwa zawadi.

Maandalizi bado yanaendelea jana tulipata bahati ya kuwatembelea MBEYA FILM ALL STAR ambao wao wanajiandaa kwa VUNJA MBAVU na IGIZO KIDOGO, na leo tutakuwa MBEYA LIVING LAB.


MUHIMU
· Kufika kwa muda
· Sweta au koti kwa ajili ya baridi
· Kiatu cha safari
· Suruali au pensi (wasichana)

 NYOTE MNAKARIBISHWA



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts