Thursday 25 September 2014

MATUKIO KATIKA PICHA SAFARI YA LAKE NGOSI

 Maeneo ya uyole ya kati kibao cha coca kilichoandikwa karibu Mbeya, mahala tulipokutana washiriki wote ili tuweze kuanza safari ya pamoja kuelekea ziwa ngosi.
Vijana kutoka MBEYA YOUTH DEVELOPMENT NETWORK (VIJANA MBEYA) Steve Mwakakeke, Kelvin Paul na Christopher Mwaipopo.
Mr. Mannaseh aliekuwa Tour guide wetu ambae kwa kweli tulimuona kama mzee lakini shughuri yake ya kupanda milima vijana wengi hawakuona ndani.
Swaiba Mswahili akiwa na Rehema Joel, na pembeni ni Mr. Manaseh wakiuangalia muinuko uliokuwa mbele yao
Ni moja kati ya vibao tulivyokutana navyo tulipoingia katika msitu wa poroto, kikiwa kimeandikwa usiingie msituni, usilime msituni, usiwinde msituni, usianzishe moto na usichunge mifugo.

 Dada yetu Happy Mmila ambae ni Mtanzania lakini anasoma katika chuo cha makelele uganda, pia ni balozi mzuri sana wa mambo ya utalii alisema lazima nifike ili niweze kuwasimulia wenzangu ili waweze kufika ziwa ngosi.

 Sehemu ya kwanza ya mapumziko ya safari yetu

 Baada ya kufika juu muonekano wa ziwa ngosi ulikuwa hivi, kiukweli ni sehemu ambayo inavutia sana na kuna ubaridi saafi
 Kelvin paul, Lwitiko Mwamasika na shark wakipiga picha ya pamoja juu ya mlima.

 Wadau wakishuka kutoka juu kuelekea mahali ziwa liliko, ilituchukua muda wa kutosha ili kuweza kuyafikia maji. baada ya kushuka tukakatiza katika msitu mnene na ndipo tukafika katika kingo za ziwa Ngosi

Christopher Mwaipopo akiwa ndani ya Hifadhi ya msitu wa Poroto.

 Ukiwa juu ziwa ngosi huonekana kama ramani ya Afrika hivyo hiki ni moja kati ya vitu vyenye muonekano wa visiwa ambavyo viko viwili.
 Matukio mbali mbali yakiendelea na wadau hawakupenda kuwa mbali na matukio karibu kila mmoja alipenda japo achukue picha ama picha za mnato kama kumbukumbu

 Washiriki mbali mbali wa shindano la kukimbia na yai likiwa juu ya kijiko, kisha kijiko kinang'atwa na meno ya mbele.

 Mshindi wa shindano la kukimbia na yai akizungumza na mdhamini wa shindano hili bwana Volustano Mdee kutoka Mbeya living Lab



Sylivester Seme akipumzika baada ya safari ndefu.


 Ripoti maalum itawajia juu ya utafiti uliofanywa na wadau waliotembelea ziwa ngosi

JE NI KWELI UKIPIGA KELELE/KUITA JINA LA MTU YEYOTE UNAPOTEA?
JE NI KWELI UKINYWA MAJI YA ZIWA NGOSI UNATOKWA NA TONSES?
JE NI KWELI UKIONGEA KINYAKYUSA ZIWA LINAHAMA?

Haya yote tutakupatia majibu baada ya kufanya utafiti katika ziwa ngosi........

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts