Tuesday 1 July 2014

MLIMA LOLEZA.

Mlima Loleza.

Mlima Loleza ni moja kati ya milima ipatikanayo mkoani mbeya, mlima huu unaonekana vizuri ukiwa katikati ya jiji. Ni safu mwendelezo wa mlima Mbeya. Umeungana na mlima Kawetele uliopo usawa wa Uyole.

Katika mlima huu kuna shughuli kadha wa kadha zinazo endelea. Shughuli hizo ni za kimaendeleo kama, Misitu ya mbao aina ya mipaina, ni kitovu cha kupokea na kutuma mionzi ya mitandao ya mawasiliano.

Wenyeji wanaopatikana katika maeneo ya mlima huo ni jamii ya Wasafwa na Wabungu. Shughuli kubwa ya wenyeji wa huko ni kilimo cha mazao ya mahindi.

Mandhari ya Mlima huo.
Katika kilele cha mlima huu kuna hali ya ubaridi wa wastani wenye upepo mwanana. Ukisimama utaweza kuona sehemu kubwa ya Jiji la Mbeya kwa uelekeo wa kusini. Na kwa uelekeo wa kaskazini magharibi linaoneka ziwa Rukwa kwa mbali. Hali kadhalika kwa uelekeo wa Kaskazini mbele ya miti ya Mipaina linaonekana kwa sehemu eneo la wilaya ya Chunya na upande wa mashariki inaonekana mwendelezo mzima wa safu za mlima kutoka Kawetele.

Safari ya kuupanda mlima loleza.
Safari ya kupanda mlima huu kwa watembea kwa miguu huanzia maeneo ya hospitali ya Rufaa Mbeya, safari huwa yenye kufurahisha kuanzia kituo namba moja hadi kituo namba kumi na tano, baada ya hapo kuna kilima kidogo ambacho baadhi ya watu huita mlima kucha ambacho kimeinuka sana hivyo kupanda kwake ni mpaka mjishikirie chini mithiri ya kutambaa ambapo asilimia kubwa ya watu hiushia hapo kwa sababu ya kuwa na muinuko mkali kidogo. 

Pia mlima huu hupandwa kwa usafiri wa magari. Usafiri huu hupitia njia ya Mbeya-Chunya na mpaka kufikia kileleni.

Karibu Mbeya, Karibu Tanzania

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts