Thursday 3 July 2014

MAAJABU YA PANGO LILILOPO KATIKA MAPOROMOKO YA MAJI KAPOROGWE.

Waswahili husema tembea uone, Haya ni maporomoko ya maji kaporogwe ni moja kati ya maeneo yenye kuvutia sana mkoani mbeya, eneo hili lipo katika wilaya ya Rungwe karibu na vijiji vya kisa na iponjola.

Muonekano wa maji ukiwa nje ya pango.

 uwapo ndani ya pango basi maji katika maporomoko haya huonekana kwa namna hii.


Ndani ya pango ukiwa pembezoni.


Katika moja ya sifa za pekee sana za mahala hapa ni kuwa na hewa safi na mwanana hujapata kuona, pia ni eneo lililozingirwa na mimeo yenye kijani chenye kupendeze kama uonavyo katika picha. Maporomoka haya ni ya mto kala, katika eneo hili kuna miamba mbayo ndani yake ni pango.

Cha kushangaza ni ukubwa wa pango hili, linauwezo wa kuruhusu watu wasiopungua hamsini (50) na wasiozidi mia moja kumi(110) kuingia ndani yake.

Kwa nini usimuliwe? Karibu sana Mbeya ujionee kwa macho yako na ujifunze mengi na kuburudika uwapo maeneo haya.




KARIBU TANZANIA, KARIBU MBEYA.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts