Wednesday, 30 July 2014

JE WAUJUA MLIMA UGALI ULIOPO JIJINI MBEYA?

Muonekano wa Mlima Ugali uwapo maeneo ya chuo cha kilimo uyole.

 Miti aina ya mipaini.

Tonny Mgombela akipumzika baada ya kupanda nusu ya mlima.

nikionesha milima ya Kawetele.
Mashamba ya chuo cha kilimo uyole yaonekanavyo.

                                                         vijiji viuzungukao mlima huu.

katika kilele cha mlima huu.

Mlima huu unanjia mbili za kuweza kuufikia, wapo wale wanaopita chuo cha kilimo uyole na pia wapo wale wanaopita maeneo ya Ituha.

Njia rahisi ya kuupanda mlima huu ni kupitia njia ya chuo cha kilimo uyole muinuko wake si mkali sana ni wa kawaida, lakini upande wa ituha umesimama sana kuliko upande wa chuo, uwapo juu ya mlima pana kibaridi safi sana.

Tulipozungumza na mmoja wa wenyeji ni kwa nini mlima huu unaitwa mlima ugali? alisema hata yeye aliikuta jamii kubwa wakiita mlima hivyo, japo mwingine alisema mlima huu kimuonekano unafanana na ugali ndio chanzo cha jina hilo.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya

Saturday, 26 July 2014

PICHA SABA[7] ZA MUONEKANO WA SAFU ZA MILIMA YA MBEYA UWAPO KWENYE NDEGE.

 







Uwapo angani [katika ndege] utaweza kuliona jiji la mbeya likiwa limepambika kwa uzuri sana, pia utaweza kuona namna ambavyo limezungukwa na milima, mashamba katika baadhi ya maeneo kama uonavyo katika baadhi ya picha.

Muonekano huu ni pale ambapo mnakaribia kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe ndipo utafurahia kuona milima ikionekana kama vichuguu kwani huwa midogo sana its so beautiful.


Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

Friday, 25 July 2014

MOJA YA CHAKULA CHA ASILI MKOANI MBEYA..


Majani ya Kitugu.
 Kitugu kikiwa kimekatwa tayari kwa kupikwa.

 Rangi ya njano ndani ya kitugu.

Jina asili ya hili jimbi ni jimbi kuu, kwa kinyakyusa linaitwa kitugu, lakini chenyewe ni kikubwa sana kuliko jimbi la kawaida, sifa ya jimbi hili ni kwamba linadumu miaka mingi sana lakini majimbi mengine hudumu kwa muda wa mwaka mmoja au miwili na kupandwa tena.  kitugu hakivunwi bali hukakatwa kipande kulingana na hitaji la familia kisha hufukiwa vivyo hivyo nacho kinaendelea kukua pasipo kuoza pale kilipo katwa.

Cha kushangaza ni pale tulipo kikuta kitugu hiki mzee alisema yeye alikikuta kikiwa kimepandwa na baba yake ambae mimi ni nyanya yangu na bado kipo na wanakula lakini pia yeye hajui ni lini kilipandwa na baba yake, ni kitu ambacho ni adimu sana na kilitumiwa kama mkombozi ama akiba ya chakula kwa baadhi ya makabila ya mkoa wa mbeya hasa wakati wa kiangazi.

Kitugu kina rangi nyingi ikiwemo nyeupe, kingine ni mchanganyiko kama lilivyo jimbi la kawaida lakini hiki kilikuwa cha njano tangu kikiwa kibichi hadi kilipopikwa hakikubadilika rangi.

Jimbi hili likiota hutoa majani yenye kamba ambayo hutambaa kama mapohola ama mboga ya maboga, hivyo basi linatakiwa kivingirishwa katika kimti chenye matawi mengi huweza kuuziba mti kabisa. ukimaliza kusoma makala hii muulize baba, mama, babu, bibi juu ya kitugu, awali atashituka na kukuuliza wapi umekipata ama kukiona.


Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Sunday, 20 July 2014

IFAHAMU BARABARA ILIYOJENGWA JUU ZAIDI TANZANIA.

Kibao kinachoeleza vipimo namna barabara hii iliyvo. 

muonekano wa kibao ukiwa usawa wa chini kidogo kutoka usawa wa barabara.

Upande wa kushoto ni barabara maeneo ya kawetele lakini kulia ni muonekano wa muinuko ilikopita barabara.

ukiwa juu utaweza kuona muonekano wa bonde la ufa kama lionekanavyo katika picha hii.

Barabara hii inaanzia standi ya mwanjelwa inapitia isanga kuelekea Chunya,  ambapo barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani kama Singida, Dodoma na Tabora. uwapo safarini alama pekee ya kukufanya utambue umefika maeneo ya kawetele ni hali ya hewa safi na mwana ambapo eneo hili limewekwa vipimo vya hali ya hewa(Airpoint).

Mahali hapa barabara ipo juu kuliko barabara zote nchini Tanzania, Eneo hili lipo barabara ya Chunya nje kidogo ya jiji la Mbeya, uwapo juu kawetele Utaweza kutizama mandhari ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, linalopitia maeneo ya mji wa mbeya, utaweza kuona Bonde la Usangu na maeneo kama Inyala, Chimala, Igurusi, Itamba, Msesule na kadhalika. pia Utafurahia sana kuiona reli ya Tanzania Zambia Railway (TAZARA) inavyolizunguka eneo hilo.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Saturday, 19 July 2014

IJUE BAADHI YA MITAA YA JIJI LA MBEYA.



Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Philip Mulugo.



Hili ni eneo la kungilia ofisi za SIDO Mbeya eneo la Block T. Jijini Mbeya.



Mbeya sasa inapendeza, hili ni eneo la kwenda Shule ya Msingi Samora, Airport Jijini Mbeya.



Hapa ni barabara inayotok eneo la Esso, Jijini Mbeya kuelekea Forest Mpya, Jijini Mbeya. Sasa ni Lami tupu



Hapa ni eneo la kuelekea chuo cha Mzumbe Campas ya Mbeya. Ni Forest ya zamani barabara ya Benki kuu.



Barabara ya Hosptali ya mkoa wa \Mbeya.







Eneo la uwanja wa ndege wa awali kabla ya unaotumika sasa wa Songwe, uwanja huu upo Jijini Mbeya eneo la Airport Mwanjelwa kwa sasa kipande kinatumika kwa kilimo kama inavyoonekana.



Hapa ni soko la Soweto Jijini Mbeya.

Chanzo: www.marymwanjelwa.blogspot.com


Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Thursday, 17 July 2014

IFAHAMU ASILI YA JINA TUKUYU.


Tukuyu Ni mji upatikanao kilomita 70 kutoka mbeya pia kilomita 61 kutoka kyela KWA wasio na uhakika au hata kwa wasio na habari kabisa, mji wa Tukuyu ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya. Ni moja ya maeneo yanayokaliwa na watu wa kabila la Wanyakyusa na ambalo linafahamika vyema kwa kilimo cha ndizi, maharage, mahindi, magimbi na kadhalika kwani hupokea mvua kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha masika na kwa sehemu kubwa zaidi ya mwaka.

Tukuyu ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani ikaitwa Neu Langenburg ("boma ndefu mpya") badala ya Langenburg ya awali iliyokaa mwambaoni wa Ziwa Nyasa ikazama chini wakati wa maji ya ziwa kupanda. Hadi leo jina la hoteli kuna hoteli iitwayo "Langiboss" inakumbuka jina la zamani. 

je asili ya mji huo kuitwa Tukuyu ni ipi?
Kulwa Mwaibale, mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya, anasema: “Eneo ambalo leo uko mji wa Tukuyu lilikuwa na miti aina ya mikuyu.  Hivyo wenyeji wa sehemu hiyo ambao ni Wanyakyusa, wakawa wanapaita mahali hapo ‘patukuju’ yaani mahali penye miti ya mikuyu.  Kutokana na lafudhi ya Wanyakyusa, kwao ilikuwa rahisi kusema ‘tukuju’ badala ya ‘tukuyu’!”
Mwaibale ambaye ni mmoja wa waandishi wa habari wakongwe nchini,  anaendelea kusema kwamba katika mwingiliano wa makabila mengi yaliyokuwa eneo hilo, wakiwemo wakoloni ambao walikuwa na majukumu ya kuweka kumbukumbu mbalimbali za maeneo nchini, neno ‘tukuju’ likabadilika na kuwa ‘tukuyu’ na hivyo kuwa jina la mji huo ulio kusini mwa Jiji la Mbeya katika barabara kuu iendayo mji wa Mbamba Bay ulio kando ya Ziwa Nyasa na nchi ya Malawi.

“Tukuyu ni jina zuri na halina matatizo ya kulitamka, japokuwa jina halisi lilikuwa ‘tukuju’ kama walivyokuwa wanalitamka watu wa asili katika eneo hilo,” anasema mwandishi huyo.

Chanzo: Global Publishertz

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts