Thursday, 17 July 2014
IFAHAMU ASILI YA JINA TUKUYU.
Tukuyu Ni mji
upatikanao kilomita 70 kutoka mbeya pia kilomita 61 kutoka kyela KWA wasio na uhakika
au hata kwa wasio na habari kabisa, mji wa Tukuyu ni Makao Makuu ya Wilaya ya
Rungwe katika Mkoa wa Mbeya. Ni moja ya maeneo yanayokaliwa na watu wa kabila
la Wanyakyusa na ambalo linafahamika vyema kwa kilimo cha ndizi, maharage, mahindi,
magimbi na kadhalika kwani hupokea mvua kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha
masika na kwa sehemu kubwa zaidi ya mwaka.
Tukuyu ilianzishwa
wakati wa ukoloni
wa Kijerumani ikaitwa Neu Langenburg ("boma ndefu
mpya") badala ya Langenburg ya awali iliyokaa mwambaoni wa Ziwa Nyasa
ikazama chini wakati wa maji ya ziwa kupanda. Hadi leo jina la hoteli kuna hoteli iitwayo "Langiboss" inakumbuka jina la zamani.
je asili ya mji huo kuitwa Tukuyu ni ipi?
Kulwa Mwaibale, mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya, anasema: “Eneo ambalo leo uko mji wa Tukuyu lilikuwa na miti aina ya mikuyu. Hivyo wenyeji wa sehemu hiyo ambao ni Wanyakyusa, wakawa wanapaita mahali hapo ‘patukuju’ yaani mahali penye miti ya mikuyu. Kutokana na lafudhi ya Wanyakyusa, kwao ilikuwa rahisi kusema ‘tukuju’ badala ya ‘tukuyu’!”
Mwaibale ambaye ni mmoja wa waandishi wa habari wakongwe nchini, anaendelea kusema kwamba katika mwingiliano wa makabila mengi yaliyokuwa eneo hilo, wakiwemo wakoloni ambao walikuwa na majukumu ya kuweka kumbukumbu mbalimbali za maeneo nchini, neno ‘tukuju’ likabadilika na kuwa ‘tukuyu’ na hivyo kuwa jina la mji huo ulio kusini mwa Jiji la Mbeya katika barabara kuu iendayo mji wa Mbamba Bay ulio kando ya Ziwa Nyasa na nchi ya Malawi.
“Tukuyu ni jina zuri na halina matatizo ya kulitamka, japokuwa jina halisi lilikuwa ‘tukuju’ kama walivyokuwa wanalitamka watu wa asili katika eneo hilo,” anasema mwandishi huyo.
Chanzo: Global Publishertz
Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania

0 comments:
Post a Comment