Friday, 25 July 2014

MOJA YA CHAKULA CHA ASILI MKOANI MBEYA..


Majani ya Kitugu.
 Kitugu kikiwa kimekatwa tayari kwa kupikwa.

 Rangi ya njano ndani ya kitugu.

Jina asili ya hili jimbi ni jimbi kuu, kwa kinyakyusa linaitwa kitugu, lakini chenyewe ni kikubwa sana kuliko jimbi la kawaida, sifa ya jimbi hili ni kwamba linadumu miaka mingi sana lakini majimbi mengine hudumu kwa muda wa mwaka mmoja au miwili na kupandwa tena.  kitugu hakivunwi bali hukakatwa kipande kulingana na hitaji la familia kisha hufukiwa vivyo hivyo nacho kinaendelea kukua pasipo kuoza pale kilipo katwa.

Cha kushangaza ni pale tulipo kikuta kitugu hiki mzee alisema yeye alikikuta kikiwa kimepandwa na baba yake ambae mimi ni nyanya yangu na bado kipo na wanakula lakini pia yeye hajui ni lini kilipandwa na baba yake, ni kitu ambacho ni adimu sana na kilitumiwa kama mkombozi ama akiba ya chakula kwa baadhi ya makabila ya mkoa wa mbeya hasa wakati wa kiangazi.

Kitugu kina rangi nyingi ikiwemo nyeupe, kingine ni mchanganyiko kama lilivyo jimbi la kawaida lakini hiki kilikuwa cha njano tangu kikiwa kibichi hadi kilipopikwa hakikubadilika rangi.

Jimbi hili likiota hutoa majani yenye kamba ambayo hutambaa kama mapohola ama mboga ya maboga, hivyo basi linatakiwa kivingirishwa katika kimti chenye matawi mengi huweza kuuziba mti kabisa. ukimaliza kusoma makala hii muulize baba, mama, babu, bibi juu ya kitugu, awali atashituka na kukuuliza wapi umekipata ama kukiona.


Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts