Tuesday, 8 April 2014

SAFARI YA DARAJA LA MUNGU NA KIJUNGU JIKO.

Haya yalikuwa maneno yaliyotuvutia sana tulipofika maeneo ya KK wilayani Rungwe.


daraja la mungu, ambalo limeundwa kwa mwamba hivyo kuwa na muonekano wa daraja.

Hapa ni juu ya daraja, ambapo tulivuka na kujionea maajabu haya ya uumbaji.



tukiwa chini karibu na maji tukishangaa uumbaji huo wa ajabu, ni sehemu moja nzuri sana. amos asajile, lusajo mwaihabi na walter marko


baada ya kutoka daraja la mungu tukaanza safari kuelekea kijungu jiko.


ni shimo lenye umbo kama chungu, maji mengi hupita hapo na kutokea upande wa pili yake.


muonekano wa kijungu jiko mkiwa juu kabla ya kushuka bondeni



Daraja la mungu na kijungu jiko ni maeneo ya kitalii muhimu sana mkoani mbeya katika wilaya ya rungwe, ili kufika kama ukitokea mkoani mbeya unashuka kyimo kijiji kitulivu (KKK) ambacho maarufu kama KK, kisha unaelekea ndani kwa umbali wa kilomita zisizo pungua 6. 

DARAJA LA MUNGU, ni daraja kama madaraja mengine lakini ni la asili kwa maana ya kwamba hakuna mkandalasi ambaye amehusika kulijenga au kutengeneza, daraja hili hupitisha maji yake kutoka mlima rungwe kisha kumwaga ziwa nyasa.

KIJUNGU JIKO, ni mwamba ulio na umbo la chungu ambao pia hupitisha maji yake kisha kuyatolea upende wa pili, kulingana na maelezo ya mwenyeji wetu yakitoka mengine hupitiliza na mengine huingia  katika shimo {imbako}.

TUPENDE UTALII WETU WA NDANI.


0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts