Wednesday, 16 July 2014

MJUE MNYAMA AJULIKANAYE KWA JINA LA NUNGUNUNGU.

Nungnungu ni wanyama wagugunaji wenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadui. Walienea katika ulimwengu wa sasa na ulimwengu wa zamani. Katika wanyama wagugunaji ni watatu kwa ukubwa, wakitanguliwa na capybara na buku. Nungu wana urefu kati ya sm 20 - 25. Uzito wao wakaribia kg 5.4 - 16. Wana umbo la duara, wakubwa na wataratibu kweli.

Nungunungu ni wanyama ambao huwa na rangi mbalimbali zikiwemo kijivu, nyeusi, kahawia ambayo imepauka kwa sababu ya rangi zake na kumfanya kuwa miongoni mwa vivutio vya utalii

Nungunungu wa dunia ya leo wanaumbo dogo (japokuwa nungunungu wa Amerika ya Kaskazini wanafikia kama sm 85 kwa maelfu na uzito wa kilogramu 18), 

Ni vigumu sana kuweza kuwaona kwa vile wanaishi kwa mashaka sana,maana mara tu wanapoonekana machoni pa watu hushambuliwa na kuwaua kwa sababu mbalimbali. Wengine huwaua kwa sababu ya kuwatuhumu kuwa wanakula mazao yao mashambani.Lakini wengine huwaua kwa sababu wanadai kuwa miiba yake ni dawa.

Nungunungu hupenda kuishi na kufurahia mazingira yenye mapori na misitu ili kujihadhali na ukatilii anaotendewa. Ni vigumu sana kumpata mnyama kama Nungunungu katika sehemu zenye nyasi fupi fupi huwa huishi kwe sehemu zenye nyasi ndefu kwa ajili ya usalama wao.

Nungunungu hula chakula ambacho mara nyingi hulimwa na kuandaliwa na binadamu huko mwituni, ambako ndio sehemu sahihi ya maakazi ya Nungunungu. Kutokana na kuharibiwa makazi yao Nungunungu hulazimika kula mazao yaliyolimwa kama mahindi, ndizi, mihogo, na mazao mengine yanayoliwa na binadamu hiyo upelekea kuwa na uadui mkubwa na binadamu na Nungunungu kuona kuwa mazingira alimo binadamu si maeneo sahihi kwa kuishi ns kuendeleza maisha yake yote. Kwa hiyo uhama na kwenda sehemu jingine.

Nungu hupatikana sana katika maeneo ya kawaida na tropiki ya Asia, Italia, Afrika na Amerika ya Kusini na Kaskazini. Nungu huishi kwenye misitu, jangwani sehemu zenye miamba, vilima na nyikani. Baadhi ya nungu wa Dunia Mpya huishi kwenye miti, lakini nungu wa Dunia wa Kale wanakaa ardhini. Nungu huweza kupatikana hata kwenye miamba kwenye ardhi yenye hata urefu wa mita 3700. Nungunungu ni wanyama wa usiku.

Nungunungu hawazaliani kwa wingi sana kama wanyama wengine wanaoishi mwituni hii ni kwa sababu ni wanyama ambao jamii huwatumia sana kwa ajili ya kitoweo pamoja na shughuli nyingine kama dawa ya asili.

Katika Tanzania inasemekana Nungunungu huwapatikana kwa wingi katika mapori mbalimbali likiwemo pori la Nyamunsi lililoko Wilayani Tarime Mkoa wa Mara. Baadhi ya Wenyeji wa sehemu hiyo wanaamini kuwa ngozi ya Nungunungu ni dawa ya watoto wadogo na hivyo waganga wengi huwawinda na kuwatumia kwa lengo la kutibu watu kutokana na imani tofauti katia jamii. Pia Nungunungu anahusishwa sana na uchawi kwani anaaminika kuwa ukimkuta njiani ni ishara ya kutokea kwa jambo fulani baya au zuri.

Nijukumu la sisi Watanzania kuhifadhi makazi ya wanyamapori kwa kuwa ni suala la sisi sote.Wanyamapori hawa ni urithi wetu,kila mmoja wetu atimize wajibu wake kwa nafasi yake ili kuhakikisha uwo wa rasilimali ya wanyamapori na matumizi yake vinakuwa enendelevu.

Chanzo: Maliasili Zetu

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya

WILAYA ZA KWANZA KULIMA CHAI NYANDA ZA JUU KUSINI MWA TANZANIA (WILAYA YA RUNGWE NA MAFINGA)


KYIMBILA ni sehemu ya ambayo ipo nje kidogo ya mji wa Tukuyu umbali wa takribani kilomita Mbili (2) imepitiwa na barabara kuu ya kwenda nchi jirani ya malawi iliyoanzia uyole wilayani mbeya na kuishia wilayani kyela, Eneo hili liinapatikana katika ukanda wa bonde la ufa,

CHAI ni zao la biashara linalostawi zaidi katika Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya na Mafinga, mkoa wa Iringa. Zao hilo kwa mara ya kwanza lilianza kupandwa katika mikoa hiyo ya nyanda za juu kusini tangu miaka ya 1960. Historia ya zao hilo inajipambanua kuwa kilimo hicho kilianzishwa mikoa ya nyanda za juu kusini baada ya hayati Mwalimu Julius Nyerere kuona nguvu kazi ya taifa ikipotea kwa kukimbilia katika migodi Afrika Kusini na Zambia wakitumika kama manamba.
Kyimbila imepakana na makandana upande wa kaskazini, upande wa magharibi imepakana na kijiji cha nkuju, upande wa mashariki imepakana na kijiji cha mpumbuli na kusini imepakana na kijiji cha ushirika na pia na kyimbila ni sehemu ya kwanza Tanzania kwa kuanza kulima chai baada ya kuonekana ni eneo la viwila na mazingira kwa zao hilo na ilikuwa mwaka 1902 baadaya ya zao hilo kustawi kwa wingi ndipo maeneo mengine wakaendelea kulima zao hilo na mzungu aliyelima chai kwa mara ya kwanza kyimbila aliitwa Williamson na aliweza kujenga viwanda vya chai mbalimbali katika maeneo ya kyimbila, msekera na chivanje na baadaya ya williamson kumaliza mkataba wa uwekezaje kampuni zingine zikawekeza na sasa chai kwa eneo la kyimbila ipo chini ya mwekezaji mtanzania mwenye kampuni ya MeTL.

Kyimbila ni moja kati ya maeneo mazuri sana kwa masomo (STUDY TOURS). Nikiwa napita maeneo haya  nliwakuta wanafunzi wa kidato cha Tatu (3) ungana nasi tutawaletea msitu upatikanao kyimbila.



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
Monday, 14 July 2014

ZIWA KINGILI (CRATER LAKE)

Muonekano wa ziwa kingili, pembeni yake kama uonavyo ni misitu.

Upande wa pembeni mwa ziwa kingili.

Ziwa kingili linapatikana umbali wa kilomita 10 magharibi mwa ipinda, kaskazini mashariki mwa kyela umbali wa kilomita 30. eneo hili ni zuri na la kuvutia sana kwani limezingilwa na msitu mdogo ambao ndani yake utafurahia kuona nyani, ndege aina mbali mbali, shughuri za uvuvi nk.

Ukipita njia ya mkato kutoka Tukuyu kwa kupita Mbambo basi utakunja kulia kwako mara baada ya kufika Ntaba sokoni. Vivyo hivyo ukitokea Ipinda basi utapinda kushoto kwako.

Ni sehemu nzuri ya kutembelea kwa sababu utaweza kujifunza mengi lakini pia mje kidogo ya eneo hili kuna kilimo cha umwagiliaji hivyo utafaidika na mengi sana

Sunday, 13 July 2014

SIRI YA JOKOFU LA KALE (MTUNGI), KUKAA KATIKA KONA YA NYUMBA.

Mtungi wa maji ya kunywa.

Mtungi ni chombo chenye umbo la duara, kilichofinyangwa kwa udongo. Mtungi ulikuwa ukitumika kutunzia maji masafi ya kunywa, kuhifadhia vyakula kama vile maharage, unga, karanga nk, baadhi ya watu walikuwa hodari hivyo waliitia nakshi sana mitungi yao kwa kuichora, kuandika maneno yenye kuvutia na vitu kadha wa kadha.

Kwa tuliokaa kijijni tunajua nyumba ya kijijini haijakamilika bila ya kuwa na mtungi, mara nyingi mtungi ulikuwa ukiwekwa katika moja ya kona ya nyumba husika kwa sababu ilionekana ni moja kati ya eneo salama. Mtungi wa maji ulikuwa unawekwa juu ya ndoo, kisha unafunikwa kwa sahani ya bati kisha juu yake kinawekwa kikombe ambacho ni maalum kwa kuchotea maji tu, sasa ulikuwa ukitaka kujua hasira ya mama au bibi ilikuwa akukute umenywea maji kile kikombe kinachokaa juu ya mtungi

Maji ya mtungi  yalikuwa ni ya baridi sana zaidi ya maji yaliyohifadhiwa katika majokofu, pia yalikuwa hayapotezi radha yake hivyo yalikuwa ni matamu sanaaaaaa,




Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.


Saturday, 12 July 2014

KILIMA CHENYE MUONEKANO WA HERUFI (C) KATIKATI YA ARDHI OEVU (WETLAND) YA IBALE.

 Muonekano wa kilima chenye herufi C iliyogeuka

 Mashamba ya wenyeji.
 Hali ya hewa ni yenye ubaridi na kwa leo palikuwa na ukungu fulani hivi.

 Ncha moja ya herufi C katikati ya wetland


Wetland ya ibale inapatikana katika halmashauri ya busokelo, wilaya ya Rungwe kata ya Lupata. Ni sehemu yenye kuvutia sana kwani  imezungukwa na vilima vilima pande zote, ndani yake kuna chanzo cha mto magubwa pia ndiko kilipo chanzo cha mradi wa maji unaohudumia kata tatu (lupata, itete na lufilyo) pia kuna shughuli za kilimo zinafanyika kama vile kilimo cha maharage, mahindi, mbaazi, bustani za mbogamboga na nyanya.

Maeneo haya yana msitu ambapo kweye msitu huu kuna hali ya matope matope na imejaaa matete  pia vijichemchem vingi vinaibuka ndan ya msitu huu ambao wanyakyusa huita (ilolo)

Eneo hili limezungukwa na vilima vitatu ambapo kilima kimoja kipopo upande wa kata ya lwangwa kingne itete na kingne lupata. Moja kati ya vilima hivyo ndiko kuna mitambo ya kupokea na kusambaza mawimbi ya simu za mkononi ya voda, tigo na airtel

Kitu kilichonivutia Zaidi ni kilima kilichopo katikati ya wetland ukiachana na hivi vilivyolizunguka eneo ambacho kina muonekano wa alama ya herufi C iliyogeuka, aisee ni pazuri kiasi kwamba nashindwa namna ya kuelezea.

Shukrani zangu za dhati kwa bwana Gerald Mwamwaja kwa kuwa mwenyeji wangu wa safari ya ibale.


Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.


Thursday, 10 July 2014

THIS YEAR 2ND INTERNATIONAL MOUNTAIN BIKE :RACE TO MATEMA FROM 27 TO 29 NOVEMBER 2014 (MASHINDANO YA BAISKELI MWAKA 2014)

The Tanzania 1 Hamisi Hussein from Arusha who finish 4th position.


Race to Matema. (2013)
A single day International Mount Bike Event: Race to Matema Held on 26 October 2013, the Race which Include 32 Cyclist Local and International starting around 0900 hrs on Isange Village Mwakaleli in Rungwe Mbeya path through Hills and Valley of Tukuyu and Kyela down to Matema Beach area where the race of 126 Kilometer ends. Congratulations to Kenyan and Arusha Cyclist who secure the top Three position, Kenya Pro Experience Cyclist David Kinjah Kibachia (Is the one who Introduce to Bike the Kenyan-born Toure de France 2013 winner Chris Froome) ,Vincent Chege and Joseph Kuria inaugurate the race for the first time and win 1st ,2nd and 3rd position in male while Sophia Adson (2nd in 2013 Tanzania National Champion) from Arusha ,Sophia Hussein(1st in 2013 Tanzania National Championship) from Arusha and Martha (3rd in 2013 Tanzania National Championship ) from Mwanza respectively win on Female Category 1st,2nd and 3rd position.

The race experience the new Talented Cyclist from different Angle of Tanzania compete with National Level Cyclist from-Arusha , Dodoma, Iringa , Mbeya, ,Morogoro,Mwanza and Zanzibar. Hussein from Arusha who is the winner of 2013 Tanzania National Champion finishing in 4th position while Masunga Duba from Mwanza who also the 2nd in 2013 Tanzania National Championship finishing 5th ,Mahenga from Mbeya town who ware run for the first time finishing in 6th Position and make Mbeya proud for their best position.
Cyclist Name ,Code Number, Nationality and Position coming soon.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.

MTAALAM WA MCHEZO HATARI WA BAISKELI.

Hili ni lingi la baiskeli ambalo alilivaa akiwa juu ya baiskeli kisha kulivua, baiskeli ikiwa imesimama bila kushikiliwa na kitu chochote.

Baiskeli amabayo mtaalamu huyu huitumia.

Akitoa maelezo aina ya michezo anayoweza kucheza akiwa katika baiskeli yake. na hapo alisema anauwezo wa kulizunguka duara la lingi hilo kwa baiskeli.

 kama utani vile akalivaa lingi lile kwa kuanzia shingoni kisha kulivua katika miguu pasipo kushuka juu ya baiskeli yake.

 Lingi linapita kiunoni
Tayari lingi liko katika miguu, na baiskeli imetulia tuli bila ya kushikiliwa na kitu chochote.

Bwana Tonny mwaipaya baada ya kuvua lingi, akaliweka kama awali kisha akakaa juu ya baiskeli kakunja four akinywa maji na baiskeli ikiwa imesimama bila ya stendi kama unavyoiona.

 Hapo anahama kutoka kiti cha nyuma kwenda kiti cha mbele.

 Alipokuwa akicheza wimbo wa mpoto waite.

Akionyesha umaridadi wake aliobobea katika baiskeli.

Bwana Tonny Mwaipaya ni mkazi wa mbeya katika wilaya ya mbozi. amekuwa akifanya maonesho yake katika maeneo mbali mbali ya Tanzania na leo hii alikuwa Dar es salaam maeneo ya magomeni Aliushangaza uma kwa kufanya vitu ambavyo hata waliokuwepo iliwawia vigumu kuamini kile walichokiona.

Tonny anauwezo wa kusimama juu ya baiskeli mguu mmoja katika usukani na mguu mmoja kliti cha nyuma kisha kuendesha baiskeli, anauwezo wa kuendesha baiskeli pasipo ya mnyololo, pia anauwezo wa kuichezea baiskeli kwa michezi mingi hujapata kuona. 



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts