Wednesday, 16 July 2014
MJUE MNYAMA AJULIKANAYE KWA JINA LA NUNGUNUNGU.
Nungnungu ni wanyama wagugunaji wenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadui. Walienea katika ulimwengu wa sasa na ulimwengu wa zamani. Katika wanyama wagugunaji ni watatu kwa ukubwa, wakitanguliwa na capybara na buku. Nungu wana urefu kati ya sm 20 - 25. Uzito wao wakaribia kg 5.4 - 16. Wana umbo la duara, wakubwa na wataratibu kweli.
Nungunungu ni wanyama ambao huwa na rangi mbalimbali zikiwemo kijivu, nyeusi, kahawia ambayo imepauka kwa sababu ya rangi zake na kumfanya kuwa miongoni mwa vivutio vya utalii
Nungunungu wa dunia ya leo
wanaumbo dogo (japokuwa nungunungu wa Amerika ya Kaskazini wanafikia kama sm 85
kwa maelfu na uzito wa kilogramu 18),
Ni vigumu sana kuweza
kuwaona kwa vile wanaishi kwa mashaka sana,maana mara tu wanapoonekana machoni
pa watu hushambuliwa na kuwaua kwa sababu mbalimbali. Wengine huwaua kwa sababu
ya kuwatuhumu kuwa wanakula mazao yao mashambani.Lakini wengine huwaua kwa
sababu wanadai kuwa miiba yake ni dawa.
Nungunungu hupenda
kuishi na kufurahia mazingira yenye mapori na misitu ili kujihadhali na
ukatilii anaotendewa. Ni vigumu sana kumpata mnyama kama Nungunungu katika sehemu
zenye nyasi fupi fupi huwa huishi kwe sehemu zenye nyasi ndefu kwa ajili ya
usalama wao.
Nungunungu hula
chakula ambacho mara nyingi hulimwa na kuandaliwa na binadamu huko
mwituni, ambako ndio sehemu sahihi ya maakazi ya Nungunungu. Kutokana na
kuharibiwa makazi yao Nungunungu hulazimika kula mazao yaliyolimwa kama
mahindi, ndizi, mihogo, na mazao mengine yanayoliwa na binadamu hiyo upelekea kuwa
na uadui mkubwa na binadamu na Nungunungu kuona kuwa mazingira alimo binadamu
si maeneo sahihi kwa kuishi ns kuendeleza maisha yake yote. Kwa hiyo uhama na
kwenda sehemu jingine.
Nungu hupatikana sana
katika maeneo ya kawaida na tropiki ya Asia, Italia, Afrika na Amerika ya
Kusini na Kaskazini. Nungu huishi kwenye misitu, jangwani sehemu zenye miamba,
vilima na nyikani. Baadhi ya nungu wa Dunia Mpya huishi kwenye miti, lakini
nungu wa Dunia wa Kale wanakaa ardhini. Nungu huweza kupatikana hata kwenye
miamba kwenye ardhi yenye hata urefu wa mita 3700. Nungunungu ni wanyama wa
usiku.
Nungunungu hawazaliani
kwa wingi sana kama wanyama wengine wanaoishi mwituni hii ni kwa sababu ni
wanyama ambao jamii huwatumia sana kwa ajili ya kitoweo pamoja na shughuli
nyingine kama dawa ya asili.
Katika Tanzania
inasemekana Nungunungu huwapatikana kwa wingi katika mapori mbalimbali likiwemo
pori la Nyamunsi lililoko Wilayani Tarime Mkoa wa Mara. Baadhi ya Wenyeji wa
sehemu hiyo wanaamini kuwa ngozi ya Nungunungu ni dawa ya watoto wadogo na
hivyo waganga wengi huwawinda na kuwatumia kwa lengo la kutibu watu kutokana na
imani tofauti katia jamii. Pia Nungunungu anahusishwa sana na uchawi kwani
anaaminika kuwa ukimkuta njiani ni ishara ya kutokea kwa jambo fulani baya au
zuri.
Nijukumu la sisi
Watanzania kuhifadhi makazi ya wanyamapori kwa kuwa ni suala la sisi
sote.Wanyamapori hawa ni urithi wetu,kila mmoja wetu atimize wajibu wake kwa
nafasi yake ili kuhakikisha uwo wa rasilimali ya wanyamapori na matumizi yake
vinakuwa enendelevu.
Chanzo: Maliasili Zetu
Karibu Tanzania,
Karibu Mbeya
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania
Ask a question
Archive
Popular Posts
-
Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI? Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyoto...
-
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini n...
-
J ami i ku b w a ku li k o j a m i i z ot e k a t i k a w i l a y a y a M b e y a n i W a s af w a . W asaf w a h uish i ...
-
Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri w...
-
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa . Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 1...
-
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, I...
-
Watu wa ndembo. moja kati ya wachezajia wa Ndembo akionesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki wake. wapiga ngoma wa nd...
-
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo. kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na...
-
Ni moja kati ya mimea ipatikanayo katika maeneo mbali mbali hususani katika mapori, mmea huu hutambaa kama mboga za maboga na ...
-
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani daki...
0 comments:
Post a Comment