Sunday, 13 July 2014

SIRI YA JOKOFU LA KALE (MTUNGI), KUKAA KATIKA KONA YA NYUMBA.

Mtungi wa maji ya kunywa.

Mtungi ni chombo chenye umbo la duara, kilichofinyangwa kwa udongo. Mtungi ulikuwa ukitumika kutunzia maji masafi ya kunywa, kuhifadhia vyakula kama vile maharage, unga, karanga nk, baadhi ya watu walikuwa hodari hivyo waliitia nakshi sana mitungi yao kwa kuichora, kuandika maneno yenye kuvutia na vitu kadha wa kadha.

Kwa tuliokaa kijijni tunajua nyumba ya kijijini haijakamilika bila ya kuwa na mtungi, mara nyingi mtungi ulikuwa ukiwekwa katika moja ya kona ya nyumba husika kwa sababu ilionekana ni moja kati ya eneo salama. Mtungi wa maji ulikuwa unawekwa juu ya ndoo, kisha unafunikwa kwa sahani ya bati kisha juu yake kinawekwa kikombe ambacho ni maalum kwa kuchotea maji tu, sasa ulikuwa ukitaka kujua hasira ya mama au bibi ilikuwa akukute umenywea maji kile kikombe kinachokaa juu ya mtungi

Maji ya mtungi  yalikuwa ni ya baridi sana zaidi ya maji yaliyohifadhiwa katika majokofu, pia yalikuwa hayapotezi radha yake hivyo yalikuwa ni matamu sanaaaaaa,




Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.


0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts