Monday, 23 June 2014
VIDEO YA BAADHI YA VIVUTIO VYA KITALII MKOANI MBEYA.
Kwa wale wapenzi wa picha za mnato (video), kipande hiki cha video kinaonyesha baadhi ya vivutio vya kitalii vipatikanavyo mkoani mbeya, picha ya kwanza inaonyesha namna maji yanavyo ingia na kutoka katika kijungu jiko (cooking pot) kilichopo katika mto kiwira.
Picha inayofuata ni ziwa Nyasa lililopo wilaya ya kyela maarufu kama Matema Beach, pembeni yake ni mitumbwi ambayo hutumiwa katika shughuri mbali mbali ikiwemo uvuvi. kisha picha ya mwisho inajumuisha ziwa Ngozi lililopo wilaya ya Rungwe katika milima ya uporoto, daraja la mungu lililopo katika mto kiwira, Kimondo kinacho patikana wilaya ya mbozi, na Matema beach kyela.
unaruhusiwa kupakua video hii kisha kushare na uwapendao.
Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya.
Sunday, 22 June 2014
ZIWA KIUNGULULU (CRATER LAKE)
Ziwa kiungululu linapatikana katika halmashauri ya busokelo wilaya ya Rungwe, liko umbali wa kilomita zisizozidi 48 kutoka tukuyu mjini. ziwa hili lipo eneo liitwalo lugombo katika kijiji cha kabembe kata ya itete umbali mdogo kutoka hospitali teule ya Itete.
muonekeno wa ziwa kiungululu, lililopo lugombo na kwa nyuma ni safu za milima livingstone iliyopo lufilyo.
Hakuna mto wowote unaoingiza wala kutoa maji katika ziwa kiungululu, ziwa hili lina samaki kiasi wakubwa kwa wadogo, ukitizama kwa mbali utaona safu za milima livingstone iliyoambaa mpaka katika kingo za ziwa nyasa.
Katika masimulizi ya kihistoria juu ya utokeaji wa ziwa kiungululu inasemekana, kulikuwa na mtu mmoja alitoka sehemu za mbali sana na kufika mahali hapa, alipofika alionekana kuwa ovyo sana kwa maana ya kwamba alikuwa mchafu sana, aliingia katika nyumba ya kwanza kuomba maji ya kunywa kutokana na hali aliyokuwa nayo ya uchafu walimkatalia, basi akasogea katika nyumba ya pili vivyo hivyo wakamkatalia na kumfukuza. lakini alipofika katika nyumba ya tatu alimkuta mama mmoja msamalia mwema ambae alimuonea huruma na kumpa maji ya kuoga, akamvisha nguo zingine na kisha kumwandalia chakula, mara baada ya kumaliza kula ndipo yule mtu akamwambia mama yule uhame mahala hapa uhamie sehemu nyingine kwa maana hapa patatokea maajabu, wale watu walipomwona mama yule anahama wakamsema na kumtukana kwa kusema kichaa anamhamisha na kumuona kama mtu asiekuwa na akili, baada ya kutii agizo lile ikawa kama pigo kwa wale watu waliokuwa wamebaki. Pakadidimia na kisha yakaibuka maji.
Masimulizi hayo yalitumika ili kutoa elimu kizazi hata kizazi kuzifanya jamii kuwa na ukarimu, maana masimulizi hayo hayo yalitumika hata katika maeneo mengine mfano kisiba, ikapu, ilamba na kingili.
lakini kijiografia inasemekana ziwa kiungululu lilitokana na mlipuko wa kivolkano mfano wa mzuri ni ziwa ngozi, kisiba n.k.
karibu sana Tanzania, karibu Mbeya.
HISTORIA FUPI YA MKOA WA MBEYA
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya
mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda
za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa
mingine ni Rukwa, Iringa na Ruvuma. Mkoa wa Mbeya ulianzishwa mwaka 1961 na ulikuwa ukijulikana kwa jina la ‘Southern Highland Province’ kwa kujumuisha baadhi
ya maeneo ya mikoa ya Iringa na
Rukwa. Mkoa una eneo la km. za mraba 63,617
Kati ya hizo km. za mraba
61,783 ni za nchi kavu na km. za mraba 1,834 ni eneo la
maji.
Kulingana na Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 1967
mkoa ulikuwa na watu 969,053, Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 Mkoa wa
Mbeya ulikuwa na jumla ya watu 2,063,328. Kufikia mwaka 2010 mkoa ulikadiriwa kuwa na watu 2,662,156.
Mkoa wa Mbeya
upo kusini magharibi mwa eneo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mkoa upo katika Latitudi kati ya 7º na 9º 31’ kusini ya Ikweta na
Longitudo kati ya 32º na 35º mashariki ya Greenwich. Mkoa unapakana
na nchi za Zambia na Malawi upande
wa kusini, Mkoa wa Rukwa upande
wa magharibi, Mikoa
ya Tabora na Singida
kwa upande wa kaskazini ambapo kwa upande wa mashariki unapakana na Mkoa wa
Iringa. Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Mbozi na Kasumulu katika Wilaya ya
Kyela, hufanya milango ya kuingilia na kutokea nchi za Zambia na Malawi.
Katika enzi za ukoloni
wa Waingereza, Mkoa wa Mbeya ulikuwa
ukijulikana kwa jina la ‘Southern Highland Province’. Mkoa ulikuwa ukiunganisha baadhi ya maeneo ya mikoa
mitatu ya sasa ambayo ni Iringa na Rukwa. Jina la Mbeya limetokana na neno la
kisafwa "Ibheya" ambalo maana yake ni chumvi, kutokana na wafanyabiashara kufika
na kubadilishana mazao
yao kwa chumvi. Mji wa kisasa wa Mbeya
ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo
mwaka 1927. Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana katika milima iliyopo karibu
na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu
kutokana na hali yake nzuri ya hewa. Mkoa huu ni moja kati ya mikoa mikongwe
tisa (9) iliyokuwepo mpaka wakati wa uhuru mwaka 1961.
Katika kipindi hicho, makabila makuu
katika Mkoa wa Mbeya yalikuwa ni
Wasafwa, Wanyakyusa, Wandali, Wasangu, Wamalila, Wanyiha, wakimbu na Wanyamwanga.
Kijiografia, Mkoa ulianzishwa katika maeneo yanayojulikana hivi sasa kama Uhindini, Uzunguni na Majengo.
Mji ulipangwa kufuatana na kawaida ya miji ya kikoloni ya Afrika Mashariki kuwa
na sehemu tatu zifuatazo;
(i) Uzunguni kama sehemu ya nyumba za Wazungu
na kando yake ofisi za serikali
(Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Polisi na Mahakama)
(ii) Uhindini
kama
mtaa
wa
biashara uliokuwa mikononi mwa
wafanyabiashara wenye asili ya Kihindi na Kiingereza;
(iii) Majengo
kama sehemu kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika
na familia zao.
Kwa upande wa masuala ya kiimani,
Mkoa ulikuwa umegawanywa kama
ifuatavyo;
(i) Kanisa
Anglikana lililokuwa dhehebu
rasmi la Uingereza
ambalo lipo chini ya eneo la
Uzunguni karibu na ofisi za kiserikali kama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mahakama.
(ii) Kanisa la Moravian la mjini
lilijengwa
eneo
la
Majengo
iliyokuwa
sehemu kwa ajili ya makazi ya Waafrika.
(iii) Kanisa Kuu Katoliki
lililokuwa maeneo kati ya Uzunguni
na Uhindini karibu na Majengo
ambalo lilihudumia Wazungu wachache
hasa Waeire na Wahindi kutoka Goa na Waafrika wachache.
Kwa upande wa masuala ya uchumi Mkoa wa Mbeya ulitegemea kilimo cha mazao ya
chakula yakiwemo mahindi, viazi vitamu, mtama, mpunga
na ndizi. Shughuli nyingine zilikuwa ni biashara na viwanda vidogo vidogo vya
kutengeneza zana za kilimo.
Kielimu, shule zilizokuwepo zililenga
hasa kutoa elimu kwa watoto wa machifu, wazungu na wahindi. Shule hizi zilikuwa
zinamilikiwa na serikali na mashirika ya dini.
Shule za serikali zilijulikana kama ‘Native Authority’ na za mashirika ya dini ziliitwa shule za
wamisionari. Waalimu wazalendo
walikuwa wachache, wengi wao
walikuwa ni wazungu. Misheni ya Rungwe ndiyo pekee iliyokuwa na Chuo cha Elimu
katika Mkoa wa Mbeya baada ya uhuru.
Kuhusu huduma za afya, jamii kwa kiasi kikubwa ilikuwa inatumia tiba za kienyeji. Hospitali zilikuwa chache
zikitoa huduma bure isipokuwa hospitali za
wamisionari.
Historia hii inapatikana katika taarifa ya mkoa wa mbeya miaka (50) ya uhuru.
karibu sana Tanzania, karibu Mbeya
karibu sana Tanzania, karibu Mbeya
KIMONDO CHA MBOZI.
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 12, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya, Tanzania.
Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.
Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8,69%, sulfuri0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Kina muonekano mithiri ya jiwe lakini ajabu yake ni pale utakapo kigonga kinatoa mlio kama wa debe tupu.
Muonekano wa kimondo hicho kilichopo mkoani mbeya, katika wilaya ya mbozi.
jiwe hili la chuma kwa ukaribu huonekana hivi.
hapo ni kama kachungu kana maji ukiyagusa ni ya baridi sana kama yametoka katika jokofu
Eneo hili wataalam wa mambo ya jiolojia walikata kipande cha jiwe la chuma hicho ili kufanyiwa utafiti.
Kimondo hiki kipo umbali wa kiasi cha kilometa 70 kutoka Mbeya mjini, kusini mwa Tanzania, katika barabara kuu ya Tanzania-Zambia, njia kuu ya kwenda Tunduma.
Hakuna anayejua kimondo hicho kilianguka lini, lakini lazima iwe kilianguka zamani sana kwani hakuna hekaya zozote kukihusu. W. H. Nott, soroveya kutoka Johannesburg, aliandika kwamba aliona kimondo hicho mnamo Oktoba 1930. Tangu wakati huo, mtaro ulichimbwa kukizunguka, na kufanya kionekane kana kwamba kimeinuliwa na kuwekwa juu ya madhabahu ya mawe. Hivyo, kimondo hicho kimebaki mahali kilipoanguka.
Watu fulani wamejaribu kukata sehemu fulani ya kimondo hicho ili kujiwekea kama kumbukumbu, lakini hiyo ni kazi ngumu sana. Mnamo Desemba 1930, Dakt. D. R. Grantham wa Chama cha Jiolojia alipojaribu kukata kisehemu cha karibu sentimeta kumi kwa msumeno, ilimchukua muda wa saa kumi! Kisehemu hicho kinaweza kuonekana katika mkusanyo wa vimondo kwenye Jumba la Makumbusho la Uingereza huko London.
Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya
Karibu sana Tanzania, karibu Mbeya
Thursday, 19 June 2014
ZIWA NYASA (MATEMA BEACH)
Ziwa
Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya
maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya
Viktoria, Nyanza na Ziwa Tanganyika
ziwa hili lina ukubwa wa kilomita za mraba 29,000, urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake. Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania. Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.
Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya hali ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa
Kutoka eneo la Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka 100, pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa .
Chanzo: KYELA Nyumbani.
kwa habari zaidi tembelea kyela nyumbani.
ziwa hili lina ukubwa wa kilomita za mraba 29,000, urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake. Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania. Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.
Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya hali ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa
Kutoka eneo la Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka 100, pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa .
Chanzo: KYELA Nyumbani.
kwa habari zaidi tembelea kyela nyumbani.
Tuesday, 17 June 2014
ZIWA MASOKO/ KISIBA
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani dakika 40 au 50 kwa gari.
Kihistoria inasemekana wajerumani walipokuwa wakifukuzwa na waingereza walitupa pesa na baadhi ya vitu vya thamani katika vita ya kwanza ya dunia.
Bwana benson mwaipopo ambae amekulia hapa alikuwa na mengi ya kutueleza ambayo ni:-
- ziwa masoko linapatikana kata ya kisiba na tarafa ya pakati, hapo kisiba palikuwa na vituo au sehemu za kuogea kama ifutavyo kulikuwa na sehemu ya masoko, resthouse, lwifwa, mibula na sehemu zingine lakini hizo sehemu zilikuwa maarumu kwa sababu zilifanyiwa uchunguzi zikaonekana zina kina kifupi cha maji lakini sehemu iliyokuwa na kina kifupi zaidi ni sehemu ya lwifwa ambako pia kabla hujafika majini kuna sehemu ina uwanja hapo ndipo wazungu walikuwa wakija kutarii na kufanya uchunguzi wake huwa wanafikia eneo hilo la lwifwa na eneo la bomani ndiko yanapatikana makaburi matatu na makaburi hayo yapo kwa ajili ya ukumbusho kwamba kuna wajerumani walikufa maeneo hayo walipokuwa wanaondolewa na wakoloni na inasadikika kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya nyoka mmoja mkubwa na mjerumani huyo nyoka alikuwa na vichwa viwili walipambana sana.
- Inasemekana kwamba katikati ya kina cha maji pana joka kubwa sana lipo chini ya maji na chungu kimoja pamoja na sanduku lililo jaa Rupia kama tujuavyo rupia ni kitu kimoja cha ajabu sana inasomekana inatumika kwa waganga wa kienyeji na huwa kama majini hivyo basi mnamo mwaka 1996 mwezi wa 8 wazungu walikuja kufanya utafiti wao waliweka mashine zao katikati ya maji ili kuweza kufanikisha kuchukua sanduku lililopo hapo, matokeo yake wakamtuma mzungu mmoja kati yao azame chini akaangalie atafunga vipi lile box la rupia akashimdwa alikuwa anaitwa Mark akaleta picha alizopiga pale chini na udongo alioleta kiujumla pana maajabu sana.
- Ifikapo saa 12 jioni katikati ya bwawa huwa panatokea mstari mmoja, unaotoka lwifwa kuelekea bomani usawa yaliko makaburi yale matatu. Huwa unakimbia kwa kasi ya ajabu ukizubaa huwezi ukauona unakuta tayari umejigawa unabaki kushangaa upande kunakuwa na mawimbi na upande kunakuwa na maji yaliyotulia bila hata chembe ya wimbi upande huo ambao hauna mawimbi kunakuwa na samaki sana japo ni vile vidogo vidogo ila vitamu sana basi upande wa pili huwa hawapatikani kwa wingi kuna wazungu walikuja mwaka 1997 wakapandikiza samaki wakubwa baada ya kugundua kuwa lile bwawa lilikuwa linaupungufu wa samaki lakini samaki hao walikuwa wakali sana wakiwaona wenyeji wanawatimua au ukiweka miguu majini unakuta wanakutafuna yani hapo bwawani panafurahisha hadi raha.
Like page yetu facebook, pia tu follow instagram kwa mbeya home of tourism
pia tuandikie maoni katika sanduku letu pembeni
Monday, 16 June 2014
RUNGWE NA MAAJABU YAKE
WILAYA ya Rungwe Jijini Mbeya ina mambo mengi ya kustaajabisha na miongoni mwa mambo hayo yapo kwenye Mto Kiwira.
Mto Kiwira ni mojawapo ya mito minne inayotoka Mlima Rungwe kupeleka maji kwenye Ziwa Nyasa. Mito mingine inayopeleka maji kwenye Ziwa Nyasa ni Lufilyo, Mbaka na Songwe, lakini kila mto una sifa za maajabu yanayotofautiana.
Mto Kiwira unatofautiana na mito mingine kwa mambo mengi yakiwamo ya kuwa mto wenye urefu wa karibu kilometa 70 kutoka chanzo chake kilichopo Mlima Rungwe hadi Ziwa Nyasa na pia upo chini ya ardhi kwa umbali wa karibu kilometa mbili kutoka usawa wa Mji wa Tukuyu ambao ni makao makuu ya wilaya hiyo.
Mto Kiwira umepewa jina hilo kutokana na matawi mengi ya mto huo kupitia karibu na Mji Mdogo wa Kiwira ambao ni maarufu kwa kuuza matunda mbalimbali kwa bei poa wilayani Rungwe. Sehemu kubwa ya maji ya mto huo yanaonekana kuwa meupe kutokana na kuwapo kwa maporomoko madogo madogo mengi yanayopitisha maji kwa kasi inayokadiriwa kuwa kilometa 50 kwa saa. Lakini pia yapo mabwawa ya mto huo yaliyotuama kiasi cha watu wegi kujiuliza kama maji yamesimama ama yanaendelea mbele. Kwa upande mwingine, mto huo pia unafanya kazi moja ya kiserikali ya kugawa mpaka wa vijiji katika Wilaya ya Rungwe, na pia unagawa mpaka wa Wilaya za Rungwe na Ileje , Kyela na Ileje kabla ya kuingia Ziwa Nyasa.
Umbile la Daraja la Mungu
Kama ilivyodokezwa hapo juu, Mto Kiwira upo chini zaidi ya ardhi ya Wilaya ya Rungwe na una maajabu mengi, lakini moja wapo ni la kuwapo kwa daraja linaloaminiwa kuwa la Mungu linaunganisha vijiji vya Lugombo na Mboyo Kata ya Lufingo , wilayani Rungwe.
Daraja hilo limeundwa kwa mwamba wa mawe ukiwa na urefu wa karibu mita 12 na upana wa wastani wa mita tatu. Ukitaka kwenda darajani hapo, ukitokea jijini Mbeya utapita barabara kuu ya Mbeya kwenda Kyela na utateremkia Kijiji cha Kyimo maarufu kwa jina la ‘KK’ ambapo utapata usafiri wa pikipiki au magari ya kukodi kukupeleka kwenye shimo la Mto Kiwira umbali wa kilometa karibu 10 kutoka barabara kuu.
Katika safari ya kwenda huko utaiona Sekondari ya Iponjola na baada ya hapo utaingia Kijiji cha Lugombo na kuikuta Sekondari ya mchepuo wa Kiingereza ya God’s Bridge ikiwa na jina hilo ili kuenzi Daraja la Mungu.
Safari itaendelea ukijionea pia Shule ya Msingi Kibwe na hatimaye ofisi ya Kijiji cha Lugombo kabla ya kuanza mteremko mkali ambao barabara imewekewa lami ili kupunguza madhara kwa vyombo vya usafiri hadi mtoni
Ukianza kuukaribia mto, utaona kwa ng’ambo majengo mengi mazuri yaliyotuama umbali wa kilometa moja chini ya miti pembezoni mwa Mto Kiwira.
Majengo hayo ni ya Chuo cha Askari Magereza Tanzania .Kwa asilimia kubwa majengo ya chuo hicho yapo pembezoni ya Mto Kiwira , lakini kabla ya kuuvuka mto kupitia daraja lillilojengwa na Serikali utapinda kushoto kuekelea kwenye Daraja la Mungu. Baada ya mita 400 hivi utalikuta daraja lingine ambalo linaelezwa kwamba lilijengwa na Warusi waliopewa kazi ya kujenga mtambo wa kufua umeme kwenye maji yaendayo kasi karibu na Daraja la Mungu.
Ukiwa kwenye daraja hilo utaliona Daraja la Mungu likiwa kusini mwa mto ambalo limeundwa kwa umaridadi wa aina yake. Daraja hilo kwa chini limejikunja kama upinde, lakini juu kukiwa na nafasi yenye upana unaotofautiana, kwani lipo eneo lenye upana wa mita tano na mita mbili. Kwa kweli ni la ajabu kwani hata maji yanavyokatisha eneo hilo yanatisha.
Kutisha kwake kunatokana na maji hayo, badala ya kunyoka kulikatisha daraja, yanaelekea kwanza kwenye mwamba uliopo mashariki na kuzunguka kuelekea kaskazini na hatimaye kuelekea kusini yakiwa na kasi ndogo chini ya daraja hilo kabla ya kupokewa tena na poroko lenye kasi linalotoa mvuke wakati wote.
Penye poromoko la maji hayo panaelezwa kwamba Serikali iliwatafuta Warusi ili wasaidie kuweka mitambo ya kufua umeme mwaka 1969 hafi 1978 walipofukuzwa kwa saa 24 bila kufanikisha suala hilo.
NIVYEMA TUKALITANGAZA MAANA NI KIVUTIO KIKUBWA CHA UTALII NA KIKAWA CHANZO KIKUBWA CHA MAPATO. CHANZO: MALIASILI ZETU via Tabia nchi Blog
Karibu Tanzania, karibu Mbeya
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania
Ask a question
Archive
Popular Posts
-
Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI? Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyoto...
-
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini n...
-
J ami i ku b w a ku li k o j a m i i z ot e k a t i k a w i l a y a y a M b e y a n i W a s af w a . W asaf w a h uish i ...
-
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, I...
-
Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri w...
-
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa . Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 1...
-
Watu wa ndembo. moja kati ya wachezajia wa Ndembo akionesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki wake. wapiga ngoma wa nd...
-
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo. kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na...
-
Ni moja kati ya mimea ipatikanayo katika maeneo mbali mbali hususani katika mapori, mmea huu hutambaa kama mboga za maboga na ...
-
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani daki...











