Thursday 19 June 2014

ZIWA NYASA (MATEMA BEACH)

Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria, Nyanza na Ziwa Tanganyika

ziwa hili lina ukubwa wa kilomita za mraba 29,000, urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake. Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania. Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.


Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.

  

Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali

 Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.

 Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.



Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya hali ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.

  
Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa

Kutoka eneo la Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka 100, pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa . 

Chanzo: KYELA Nyumbani.
kwa habari zaidi tembelea kyela nyumbani.

2 comments:

  1. hakika nimepapenda hapo mahali natamani siku moja nifike nijionee kwa macho yangu.........niwatakie kazi njema.

    ReplyDelete

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts