Saturday 16 May 2015

VAZI LA KALE LA WANYAKYUSA HILI HAPA

Muonekano wa pembeni wa Kikobhole

Muonekano wa pembeni wa kikobhole

‪‎KIKOBHOLE‬ ni vazi lililokuwa linatengenezwa kwa kutumia Magome ya miti (ganda la mti) lilitengenezwa kwa miti maalum aina ya MPANDAPANDA na ni moja kati ya vazi lililokuwa linavaliwa miaka ya nyuma na wazee wetu, vazi hili lilikuwa linavaliwa kiunoni kwa mfano mzuri ni kama tuvaavyo mkanda wa suruali kisha lyabhi linafuata.

‪‎LYABHI ‬pia lilitengenezwa kwa gamba la miti na lilikuwa linakuwa refu kisha linapita katikati ya mapaja ili kuziba sehemu za siri. Vali hili tulilipata kwa mzee mmoja wilaya ya Rungwe halmashauri ya busokelo vazi hili tulilikuta katika jamii ya wanyakyusa mzee huyo akasema wapo wazee mpaka sasa ambao nguo ya ndani wanaiita lyabhi. Kwa sasa limehifadhiwa ofisi za Uyole cultural tourism enterprises kwa mambo mengine waweza kutembelea ofisi yao iliyopo uyole ya kati karibu na neema sanitarium clinic.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts