Saturday 16 May 2015

KAMATI YA UTALII MKOA WA MBEYA WATEMBELEA VIVUTIO VYA KITALII

 Kamati ya utalii mkoa wa Mbeya wakiwa eneo la kijungu jiko, KIJUNGU JIKO, ni mwamba ulio na umbo la chungu ambao pia hupitisha maji yake kisha kuyatolea upande wa pili, kulingana na maelezo ya wenyeji wetu walisema maji yakitoka juu hupitiliza na mengine huingia katika shimo na yakiingia katika shimo yana kaa kwa muda wa siku saba (7).

 Picha ya muonekano wa kijungu jiko na namna ambavyo maji yanaingia mahala hapa.

Debora Ndagamsu kutoka uyole cultural tourism enterprises, akimueleza Mwandishi Mwakyembe juu ya jiwe hili ambalo liko juu ya daraja la mungu ambapo wenyeji husema latumiwa kama kumbukumbu ya mtu mwenye asili ya india aliekufa hapo 08/02/1972 kwani jiwe hili limeandikwa 8-2-72 kwani watu wengi wenye asili ya india hutembelea hapo na kupiga picha.

 moja kati ya wawakilishi wa kamati ya utalii mkoa dada Judica ambaye pia ni katibu wa wanyama pori mkoa akiwa katika pozi ziwa nyasa

DARAJA LA MUNGU, ni daraja kama yalivyo madaraja mengine na lina muonekano wenye mfano wa upinde wa mvua lakini kitu pekee kinacholifanya daraja hili kuwa tofauti na mengine ni daraja la asili kwa maana kwamba hakuna mkandalasi au mtu ambaye amehusika kulijenga au kutengeneza, daraja hili hupitisha maji yake kutoka katicha chanzo cahke kilichopo mlima Rungwe kisha kumwaga maji yake ziwa nyasa.

Safari ya kutembelea vivutio vya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kamati ya utalii ya  mkoa na kuratibiwa na watu wa hifadhi ya rungwe, pia katika msafara huu kulikuwa na mtu wa uyole cultural tourism enterprises.

Walianza kwa kutembelea KIJUNGU JIKO kisha wakaenda DARAJA LA MUNGU na mwisho ikawa ni MATEMA BEACH, Lakini pia walipokuwa kyela waliona msitu wa asili ambao ulitumiwa na wajerumani kunyongea walemavu wa viungo, Msitu huu unaitwa katago katika kijiji cha Kikusa. yapo mengi walioyaandaa baada ya safari hiyo hivyo wakazi wa mkoa wa Mbeya tukae mako wa kula kwa mambo mazuri yajayo.

Kuna Baadhi ya mambo ambayo kamati ya utalii mkoa imeyagundua ambayo ni pamoja na kibao chenye kuonyesha uelekeo wa ziwa ngozi kimekosewa kimeandikwa ni mita kumi (10) kufika ziwani badala ya kilomita nne (4), pia KK kipo kibao chenye kuonesha iliposhule ya gods bridge na si cha kuonesha lilipo daraja la mungu, hivyo wameahidi kuyashughurikia mambo yote hayo.

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts