Sunday 12 October 2014

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) WAHIMIZA WANANCHI KOTE NCHINI KUSHIRIKI KATIKA UFUGAJI WA NYUKI ILI KUONGEZA VIPATO VYAO NA KUCHANGIA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA.

Hayo yamesemwa na Afisa Ufugaji Nyuki Mwandamizi wa wakala huo Bw. Steven Msemo leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuhamasisha jamii kushiriki katika ufaugaji wa nyuki.

Akifafanua Msemo amebainisha kuwa mizinga ya nyuki takribani 14,000 imetengenezwa na kugawiwa wananchi wanaoishi jirani na Misitu ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kukuza sekta hiyo.

“Wakala wa Huduma za misitu Tanzania kama Taasisi inayo mizinga 3,870 iliyo katika manzuki mbalimbali katika kanda saba na katika mashamba ya miti kwa lengo la kuzalisha na sehemu ya mafunzo kwa jamii “alisisitiza Msemo

Katika kuwajengea uwezo wananchi Msemo amebainisha kuwa Wataalamu wa ufugaji nyuki wamekuwa wakiwajengea uwezo wananchi kwa kuwapa mbinu za kusimamia makundi ya nyuki na kuzalisha malkia ili kuondokana na mazoea ya kutundika mizinga na kuacha hadi kipindi cha mavuno.

Aidha, Wakala umekuwa ukihamasisha asasi zinazojikita na kutengeneza vifaa vya ufugaji nyuki kuzingatia utaalamu na vipimo vya mizinga.

Tanzania ni moja kati ya nchi zenye utajiri mkubwa wa makundi ya nyuki yenye uwezo wa kuzalisha asali na mazao mengine ya nyuki mfano Nta,Gundi ya nyuki na chavua.

Chanzo: Mali Asili Zetu

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts