Sunday 12 October 2014

CHANZO CHA MAJI NGAZI SITINI (60)


 Hapa  ndipo tunapoingilia na ndipo mahali zilipoanzia Ngazi sitini (60) zinazoelekea katika chanzo cha Maji NGAZI SITINI (60), kushoto na kulia ni miti ambayo imeshonana na kuweka ukuta wa maua uliofanya mahali hapa kuwa na mvuto wa aina yake.

Wadau wa utalii nlioongozana nao kuelekea katika chanzo cha maji NGAZI SITINI (60) Bwana Kelvin Paul (kushoto) na Lwitiko Mwamasika (kulia)wakiwa wamesimama katika lango la kuingilia katika chanzo hicho ambalo linafungwa muda wote ili kulinda usalama wa maji haya.

 Bwana Kelvin Paul na Lwitiko Mwamasika wakiwa katika zoezi la kuzihesabu Ngazi ili kuthibitisha kama ni kweli ziko sitini (60), mara baada ya kuzihesabu tukakuta zinatimia idadi hiyo hiyo ya sitini (60).
 Na huu ni moja ya muonekano ya msitu upatikanao katika chanzo hiki, kiukweli ni wenye kupendeza na rangi yake ni kijani kibichi.

 Na huu ni upande wa pili wa msitu huu, ambao umeshonana sana.

Mara baada ya kutoka katika kile chanzo cha maji NGAZI SITINI (60) tukasonga mbele zaidi ambapo tulikuta bomba hii ambayo imetoka katika chanzo asilia na maji yake ni masafi, ya baridi, na ni matamu sana, na hapa ni Bwana lwitiko akikinga maji ya kunywa ili tuendelee na safari.

Katika vyanzo vya maji tulivyopata bahati ya kuvitembelea ikiwemo ibale na izumbwe hiki ndicho chanzo cha maji ambacho kimetunzwa na kulindwa kwa hali ya juu sana, ukiwa katika mazingira ya karibu hata kabla hujafika katika zile ngazi unakuta mazingiza yake ni safi na yenye kupendeza sana kwani unafanywa usafi kila siku na hatukukuta aina yoyote ya takataka.

Chanzo hiki cha maji kinapatikana katika njia ielekeayo Ituha kwa kuingilia Ilomba.

Tuyatunze mazingira Yetu kwa afya zetu.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts