Thursday, 14 August 2014

SHULE YA MSINGI KONGWE ILIYOJENGWA MWAKA 1919.


 Vyumba vitatu vilivyokuwa vimejengwa na serikali ya mkoloni.

block hii ndiyo iliyojengwa na mkoloni.

Mwalimu mkuu Mr. Kilembe Isaack 

Baadhi ya wanafunzi niliowakuta wakati wa mapumziko ya mchana.

 Majengo ya vyoo vya wasichana.

Majengo ya vyoo vya wavulana.

 Kibao cha shule kinachoonesha mwaka wa kujengwa shule 1919.

Shule hii inaitwa shule ya msingi tukuyu, inapatikana halmashauri ya wilaya ya Rungwe katika mji wa Tukuyu. ilijengwa na serikali ya wakoloni mnamo mwaka 1919, ni shule ya pili baada ya ile iliyoko amani mkoani Tanga, walimu wakuu waliowahi kuitumikia shule hii ni pamoja na Mlm M. Mwakibinga 1976-1979, Mlm Mbonde 1980-1981, Mlm Mwamundela 1981-1984, Mlm Tm Mwakasege 1984-1990, Mlm M andrew 1991-1993, Mlm N Madaraka 1993-1994 , Mlm Mashaka 1994-2005, Mlm Kasala 2005-2005 alikaa muda wa takribani miezi miwili, Mlm Kilembe Isaack 2005 mpaka sasa.

Majengo yaliyojengwa na serikali ya kikoloni ni vyumba viwili vya kusomea na chumba kimoja kilichokuwa ofisi pamoja na vyoo vyenye matundu 26 ya wanawake 13 na wavulana 13, cha ajabu alichosema mkuu wa shule ni kwamba vyoo havijawahi kujaa hata siku moja.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya. 








0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts