Tuesday 8 July 2014

HISTRORIA YA WASANGU

Wasangu ni watu ambao wametokana  na jamii za Kihehe, Kisafwa, Kibena, Kinyakyusna kidogo jamii ya Kingoni. Jamii zote hizi, isipokuwa Wangoni, ni jirani za Wasangu, na kwa jumla Wasangu walikuwa ni watu ambao walijulikana sana katika nyanda za juu za Kusini katika karne ya 18 na karne ya 19. Mali kadhalika walikuwa ni jamii iliyokuwa na nguvu nyingi sana ya utawala na kivita. Hawa watu walikuwa wanaishi sehemu ya llamba iliyo karibu maili 60 Kaskazini ya Utengule kabla  ya  kuja  Waarabu  na  Wajerumani,  na  kila  mahali  walipofanya  maskani  yao  walipaita "Utengule", mahali paamani.

Waarabu walipokuwa wanaingia katika nchi ya Usangu waliingia kufanya biashara. Hawa Waarabu  walikuwa  wanauza  nguo, magobole,  baruti na shanga.  Kutoka kwa Wasangu,  Waarabu walipata meno ya tembo. Hapo awali mbuga zote za Usangu zilikuwa na wanyama wa kila aina na ndovu walienea kila mahali katika mbuga hizi za Usangu, kwa hiyo ilikuwa rahisi sana kwa Wasangu kuwaua tembo na kupata meno yao ill wayauze kwa Waarabu.

Biashara nyingine kubwa ambayo ilikuwa inafanywa na Waarabu katika mbuga hizi za Usangu ilikuwa biashara ya utumwa. Wasangu walikuwa ni watu ambao walijua namna ya kupigana vita sawasawa na kwa kuwa walikuwa na chifu wao mmoja tu ilikuwa rahisi kwao kuungana pamoja na kufanya jeshi moja kali na lenye nguvu sana kuliko jamii zingine walizopakana nazo ambazo zilikuwa hazina utawala mmoja kama vile Wanyakyusa, Wasafwa na kadhalika. Lakini Wahehe na Wakimbu walikuwa na utawala mmoja sawa kama Wasangu walivyokuwa.

Kwa kuwa utawala wa Wasangu ulikuwa na nguvu na umoja mkubwa, waliweza kupigana vita kwa nguvu moja na jamii zingine zilizokuwa  jirani nao. Chifu Merereambayndiye aliyekuwa mtawala wa Wasangu, alikuwa mtawala shupavu na mpenda raia wake. Kwa kuwa alikuwa anapata silaha bora toka kwa Waarabu alipowauzia meno ya tembo, aliweza kuwashinda maadui zake bila taabu kubwa na mateka waliuzwa kwa Waarabu wafanya biashara ya utumwa. Hasa Merere aliwauza utumwani watoto wa Kisafwa na Kihehe ambao aliwateka wakati wa vita. Uwezo wake Merere katika kupigana na jirani zake ulisaidiwa sana na ushauri aliokuwa anaupata toka kwa wazee wa Kisangu na pia toka Mbaluchi ambaye alikwenda Usangu na kuwa Mshauri Mkuu wa Vita wa Chifu Merere I ambaye yaaminiwaaliingia nchi ya Usangu kati yamwaka1878 na mwaka1880. Mbaluchi (Mburushi) huyu aliitwa Jemadariambaye kufika kwake Utengule/Usangu kulisababisha Wabaluchi (Maburushi) wengine kuja Usangu na kuanza shughuli za kilimocha mpunga (angaliachini ya kilimo hapachini). Wasangu wenyewe wanasimulia kuwa Waarabu walianza kuingia nchi ya Usangu wakati wa utawala wa Chifu Njali aliyewazaa akina Merere, siri na kupita huko. Si njia ya kutoka pwani tu iliyohatarishwa na Wasangu ball hata njia ya kuelekea nchi ya Wabemba kuelekea Zambia ilitiwa msukosuko.

Mara kwa mara Wasangu waliuteka utawala wa Kiwele uliokuwa sehemu ya kati ya Ukimbu ambao ulikuwa njiani Kusini ya Tabora. Mara baada ya Chifu Kilanga kutawala katika nchi ya Ubungu, Wasangu walimshambulia katika mwaka wa 1856 1857 wakimsaidia ndugu yake Kaf- wimbi, na ingawa Wasangu walishindwa, Kafwimbi alitorokea nchi ya Usangu tena.


Kati ya mwaka 1859 wakati Bwana Burton alipoondoka Afrika ya Mashariki na mwaka 1866 Tippu Tip alipotembelea reli ya Usangu chifu Muigumba akafariki wakati akipigana na Wahehe. Binini, ndugu ya Mihwela alikuwa amejifunza sana maarifa ya kupigana vita, na kwa kuwa alikuwa na ari kubwa ya kutaka kutawala Uhehe nzima. Wakati fulani karibu ya miaka ya 1860 alifanya vita na Wasangna alifanikiwa  kuviteka vijiji vingi sana na kuwateka  wanawake  na mifugo yao. Binini mwenyewe alimwua kiongozi wao Muigumba na akachukua jina lake na kujiita yeye mwenyewe Munyigumba kama ukumbusho wa ushindi wa kuwatawala Wahehe wote. Huyu Binini (Munyigumba) ndiye aliyekuwa baba wa chifu Mkwawa na ndiye chifu mkuu wa kwanza wa Wahehe wote.

Baada ya kifo cha Muigumba vita vikali sana vya urithi wa utawala vikatokea na mjukuu wake Muigumba kwa jina Merere Towelamahamba akatokea kuwa mshindi na akawaua jamaa zake wengi sana ambao alishindana nao katika kurithi utawala. Ugomvi wa urithi wa utawala uliwadhoofisha sana Wasangu katika kupigana vita na majirani zao.


Kati ya mwaka wa 1866 na mwaka wa 1872 Wasangu wakatokea jamii yenye nguvu sana chini ya chifu Merere wa kwanza kuliko hapo awali, na wakawashambulia majirani zao na kuziteka nchi zao zote hasa upande wa Mashariki Kusini na upande wa katikati wa nchi ya Wakimbu. Wak&ti huu Wasangu walikuwa wamefikia kilele cha nguvu zao na hakuna jamii nyingine yoyote iliyoweza kuikabili jamii ya Kisangu katika pande hizo za Tanzania.

Katika mwaka wa 1867 Bwana Livingstone aliambiwa na Waarabu katika nchi ya Ubungu kwamba Wasangu walikuwa ni wapole kwa wageni wowote, na kwamba Merere mara nyingi alifanya mashambulizi kwa machifu wa jirani ili ateke mifugo na watumwa na kuwauza kwa wafanya biashara wa Kiarabu. Katika mwezi wa Agosti Bwana Livingstone alisikia habari nyingi zaidi za kupendeza kuhusu chifu Merere na alichelea kuwa huenda akaharibiwa na Waarabu. Walakini katika mwaka w1871 habari zikafika Mayema kwamba Merere kisha kosana na Waarabu akiwatuhumu  kwamba walikuwa wanafanya njama ya kumshambulia ili Goambari, mmojawapo wa Wajukuu wa Muigumbaweze kutawala. Kwa ajili ya sababu hii Merere akawashambulia Waarabu na marafiki zao wote. Akamwua Mwarabu mmoja naakawanyang'anya Waarabu wenginemali yote waliyokuwa nayo.


Wakati huu Amrani Masudi akajitokeza kwenye uwanja wa vita. Amrani alikuwa ni Mwaarabu toka Zanzibar wakati Zanzibar ilipotawaliwa na Waarabu. Tanzania Bara ilikuwa inatawaliwa na machifu mbalimbali wa jamii mbali mbali na Waarabu waliokuwa wakiishi Tanzania Bara walikuwa wafanya biashara tu sio watawala. Kwa jinsi hii Amrani hakupendelea utaratibu huu, kwa hiyo akaamua kuwafanyia vita machifu wote wa Tanzania Bara na kuwafanya watu wote wawe chini yake ili baadaye waweze kumleteamenoyatembo bilaya kuyalipiachochote.

Wakati Amrani Masudi alipofika Tabora akaambiwa kuwa kuna machifu wawili wenye nguvu sana ambao walihatarisha misafara yote ya biashara ya Waarabu na kuwatoza kodi kubwa kabla ya kuwaruhusu kupita katika nchi zao. Machifu wenyewe ni Nyungu-ya-Mawe wa Kiwele katika nchi ya Ukimbu na Merere wa Usangu. Lakini chifu wa hatari kabisa na mwenye nguvu zaidi kuliko mwen- zake alikuwa Merere. Baada ya kupata habari hizo, Amrani akalichukuwa jeshi lake na akaomba kuongezewa askari toka kwa machifu waliomwogopa kupigana naye ili aende na jeshi kubwa la kuweza kumshambulia Merere vilivyo. Alipoondoka Tabora, alipita Ngulu, Unyangwila, Itumba, Kipembawe na Igunda mpaka akafika Usangu. Maluteni wake walipita Ukonongo, Isamba, Wikangulu, Ubungu na Uguruke. Wengine walipitia Ugogo. Kila chifu wa sehemu za Magharibi na kati na Kusini ya Tanzania alitoa kwa Amrani askari wa kumsaidia katika vita kati yake na Wasangu. Lakini Nyungu-ya-Mawe hakutoa hata askari mmoja wa kumpa Bwana Amrani.

Chanzo ni safarilands.org katika muendelezo wa makala yao ya jamii ya wasafwa.



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.


0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts