Wednesday 9 July 2014

AJABU YA MTI AINA YA MPANDAPANDA ULIOPO NJISI, LUPATA.

Majani ya mti wa mpandapanda.

 
nyuma ya mpanda panda ni migomba.

 chini ya mti kukiwa hakuna nyasi hata moja.

 kibao kinachoonesha tarehe, mwezi, mwaka wa uzinduzi wa boma la njisi.

MPANDAPANDA ni miongoni mwa miti mikubwa sana na mipana katika Halmashauri ya Busokelo, wilaya ya Rungwe. miti hii inasemekana ilipandwa na nyanya zetu, ikiwa kama sehemu ya mikutano, kufanyia ibada/ kuabudia na kufanyia shughuri mbali mbali za kimila.

Miongoni mwa miti hiyo ni ule unaopatikana katika kijiji cha NJISI, kata ya lupata. Mti huu ulianza kutumiwa kama BOMA 7. 8. 1948 na meya wa kwanza ni hayati Mwinosyege Mwakalebela, na chifu akiwa Robert Mwanyilu. (boma ni sehemu ambapo ngoma za asili za kinyakyusa hufanyikia yaani LING'OMA) 

Mti huu una majani mapana sana pia juu umesambaa sana kiasi kwamba hutengeneza kivuli kikubwa na huwa kizuri chenye hali ya hesa safi sana, lakini ajabu yake ni kwamba chini ya mti huu huwezi kukuta nyasi hata moja, na mti huu huwa na umbo la duara kwa sehemu kubwa.

Kwa miaka ya hivi karibuni ngoma zilizokuwa zikichezwa pale zilivunjika baada ya watu walio wengi kujihusisha na masuala ya kidini, mpaka hivi sasa mti huo umebaki kuwa kituo cha mabasi kijulikanacho kama MPANDAPANDA, kituo cha kukusanyia mazao mama kama chai na ndizi, pia watoto wamefanya ni uwanja wa michezo ya mpira wa miguu kama kangu, matekwa, kombolela, na aiyeba.



Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.




0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts