Tuesday, 8 April 2014
SAFARI YA DARAJA LA MUNGU NA KIJUNGU JIKO.
Haya yalikuwa maneno yaliyotuvutia sana tulipofika maeneo ya KK wilayani Rungwe.
daraja la mungu, ambalo limeundwa kwa mwamba hivyo kuwa na muonekano wa daraja.
Hapa ni juu ya daraja, ambapo tulivuka na kujionea maajabu haya ya uumbaji.
tukiwa chini karibu na maji tukishangaa uumbaji huo wa ajabu, ni sehemu moja nzuri sana. amos asajile, lusajo mwaihabi na walter marko
baada ya kutoka daraja la mungu tukaanza safari kuelekea kijungu jiko.
ni shimo lenye umbo kama chungu, maji mengi hupita hapo na kutokea upande wa pili yake.
muonekano wa kijungu jiko mkiwa juu kabla ya kushuka bondeni
Daraja la mungu na kijungu jiko ni maeneo ya kitalii muhimu sana mkoani mbeya katika wilaya ya rungwe, ili kufika kama ukitokea mkoani mbeya unashuka kyimo kijiji kitulivu (KKK) ambacho maarufu kama KK, kisha unaelekea ndani kwa umbali wa kilomita zisizo pungua 6.
DARAJA LA MUNGU, ni daraja kama madaraja mengine lakini ni la asili kwa maana ya kwamba hakuna mkandalasi ambaye amehusika kulijenga au kutengeneza, daraja hili hupitisha maji yake kutoka mlima rungwe kisha kumwaga ziwa nyasa.
KIJUNGU JIKO, ni mwamba ulio na umbo la chungu ambao pia hupitisha maji yake kisha kuyatolea upende wa pili, kulingana na maelezo ya mwenyeji wetu yakitoka mengine hupitiliza na mengine huingia katika shimo {imbako}.
TUPENDE UTALII WETU WA NDANI.
CHAKULA CHA PAMOJA MCHANA NA MICHEZO KADHAA BEACH,
Safari yetu ilianza mnamo mida ya saa sita mchana kwa kukutana
wadau wote maeneo ya ubungo Dar es salaam ili kuanza safari yetu pamoja,
Tulipofika tukakaa pamoja kwa ajili ya kupata chakula cha
mchana, ambacho wengi walipendekeza tule chakula cha asili kama kuenzi
busokelo MIHOGO, tunamshukuru alietuhudumia maana alituhudumia
vizuri sana.
Michezo kadhaa ilichezwa ikiwemo mbio fupi za majini na
mchangani, ambapo mshindi alikuwa Aswile Mwakapemba,
Wadau wakiwa katika pozi tofauti za kifuraha zaidi.
katika muonekano tofauti.
Frank Kapyungu, Lusajo Mwaihabi na Musa Otete wakiwa wamefurahiiiiiii......
hivyo ndivyo ilikuwa siku yetu, kwa maelezo zaidi unaweza kulike page yetu ya facebook BONYEZA HAPA
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Welcome
Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the
world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA
Tanzania
Ask a question
Archive
Popular Posts
-
Tuanze kwa kuangalia nini maana ya neno ASILI? Neno asili kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:3) ni jinsi kitu au jambo lilivyoto...
-
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini n...
-
J ami i ku b w a ku li k o j a m i i z ot e k a t i k a w i l a y a y a M b e y a n i W a s af w a . W asaf w a h uish i ...
-
Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na Naibu Waziri w...
-
Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa . Kinakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 1...
-
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, I...
-
Watu wa ndembo. moja kati ya wachezajia wa Ndembo akionesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki wake. wapiga ngoma wa nd...
-
Kwa mbali ni Msitu wa Iganjo ambao hutumika kama sehemu ya matambiko iliyoko huko igawilo. kulia ni Muwakilishi John Chilambo, na...
-
Ni moja kati ya mimea ipatikanayo katika maeneo mbali mbali hususani katika mapori, mmea huu hutambaa kama mboga za maboga na ...
-
Ziwa Masoko/ kisiba liko mkoani mbeya katika wilaya ya Rungwe umbali wa kilomita 19 kutoka tukuyu mjini pana mwendo wa takribani daki...