Saturday, 2 August 2014

DARAJA LA MUNGU IZUMBWE

Muonekano wa daraja ukiwa juu lakini ukiangalia kwenye maji.

 Sehemu ambayo maji hupita .

 Mti ulioota katika mwamba huo na una mizizi mikubwa sana.

 Maji ya mto huo, ni machache sana lakini kipindi cha mvua huwa mengi.

Ibrahim Kikoti, Lusajo Mwaihabi na wenyeji wakipeana maelezo juu ya daraja hili.



Daraja la mungu Izumbwe linapatikana katika wilaya ya mbeya vijijini kijiji cha Izumbwe, ili kuweza kufika hapa unafika mbalizi kisha unakunja katika njia ielekeayo Umalila, ukifika katika kanisa la moravian usharika wa Izumbwe kuna njia ielekeayo kushoto mbele kidogo ndipo lilipo daraja hili.

Katika daraja hili magari ya aina zote hupita ambayo ni makubwa kwa madogo, njia moja yaelekea kijiji jirani na njia nyingine inatokea uwanja wa ndege wa zamani.

Ni mahali pazuri sana kwa kutembelea kwani utajionea daraja hili ambalo hakuna mkandarasi yoyote aliyehusika katika kulijenga. kwa sababu limetokana na mwamba ambao umeunga pande mbili na kuwa daraja.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya

0 comments:

Post a Comment

Welcome

Travel makes one modest, You see what a tiny place you occupy in the world. This page is dedicated to promote tourist attractions of MBEYA Tanzania

Ask a question

Name

Email

Question

Submit

Popular Posts